28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

HESLB yataka uthibitisho wa vifo walionufaika mikopo

Leonard Mang’oha -Dar es salaam

BODI ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imewataka wazazi, walezi, ndugu na wadhamini wa wanufaika wa mikopo waliofariki wakiwa masomoni au baada ya kuhitimu kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha vifo vyao ili waondolewe katika orodha ya wadaiwa.

Taarifa ya bodi hiyo iliyotolewa jana ilieleza kuwa kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya Mikopo Sura ya 178 inaipa mamlaka ya kufuta mkopo wa mnufaika aliyefariki dunia.

Taarifa hiyo ilizitaja nyaraka zinazoweza kuwasilishwa zikiwa zimethibitishwa na kamishna wa kiapo au mamlaka inayozitoa kuwa ni pamoja na nakala ya cheti cha kifo, nakala ya kibali za mazishi na barua kutoka kwa mtendaji wa kijiji inayothibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Nyaraka nyingine ni barua kutoka katika chuo alichosoma au mwajiri wake na nakala ya tangazo la kifo lililotolewa kwa umma kupitia gazetini.

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa nyaraka hizo zinaweza kuwasilishwa  kwa bodi hiyo pamoja na barua kupitia anuani ya mkurugenzi mtendaji wa bodi.

“Aidha, tunawataarifu wazazi, walezi, ndugu na wadhamini kuwa HESLB imepokea baadhi ya majina wa wanufaika waliofariki dunia kutoka vyuoni ambayo inapatikana katika tovuti ya HESLB.

“Wazazi, walezi, ndugu na wadhamini wao wanashauriwa pia kuwasilisha nyaraka kama ilivyoelekezwa,” ilisema taaarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles