Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM
MWIGIZAJI na mwimbaji wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Hemedy Suleiman ‘Hemed’, amesema kuwa atapambana kuhakikisha anakuwa baba bora kwa mtoto wake.
Msanii huyo amebarikiwa kupata mtoto wa kiume ambaye amempatia jina la Marley.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Hemed alisema lengo lake ni kuwa mfano wa kuigwa na vijana, wasanii wengine wenye malengo ya kupata watoto.
“Nitapambana kuwa baba bora mwenye kuonyesha mfano kwa wengine, mara nyingi nikimuangalia mwanangu napata nguvu za kuendelea kujituma zaidi,” alisema Hemed.
Hemed alisema anajivunia kuwa baba, kwani anaendelea kushuhudia wasanii wengi ambao ni mastaa nje ya nchi wakiwalea na kuwatunza watoto wao kwa furaha, huku wakiwawekea malengo makubwa ya siku za baadaye.