27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

HAZINA YAONGOZA MOCK WILAYA YA KINONDONI

Na Mwandishi Wetu

-DAR E S SALAAM

SHULE ya Msingi Hazina ya jijini Dar es Salaam, imefanikiwa kuwa ya kwanza kwa Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam,  katika matokeo ya mitihani ya majaribio (Mock) ya darasa la saba kati ya shule 135.

Matokeo yaliyotangazwa na Ofisa Elimu wa Wilaya Kinondoni, Kiduma Mageni yanaonesha kuwa shule ya Hazina pia imefanikiwa kuingiza wanafunzi kumi bora kwa upande wa wavulana na kumi bora kwa upande wa wasichana.

Wavulana waliofanikiwa kuingia kumi bora ni Perfect Ndyetabula,, Abdurahim Sagin, Hamza Almas, Maxmbwana Max, Phinny Murungu, Walter Kiunsi na Hafidh Mohamed, Derick Ignas Menelick Sanga na Brighton Lyatuu.

Kwa upande wa wasichana waliofanya vizuri aliwataja kuwa ni Abeer Ally, Chipwe Ramson, Florensiana Simon, Ashine Mohamed, Cherish Narcis, Safina Mzuanda, Sandra lema, Evoduia Mayombo, Leyla Sagin, Najra Kimaro na Shufaa Juma.

Akizungumzia siri ya mafanikio ya shule yake, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Patrick Cheche, alisema kujituma kwa walimu na ushurikiano ambao wamekuwa wakiupata kwa uongozi wa shule na wanafunzi ndiyo kitu wanachojivunia.

“Walimu wanafanyakazi kwa moyo sana, wazazi wa wanafunzi wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri sana kwa shule na uongozi wa shule unawajali sana walimu, hayo kwa pamoja yamekuwa yakisaidia ufaulu wetu kuwa juu mwaka hadi mwaka,” alisema Mwalimu Patrick

Aliwapongeza wanafunzi kwa mafanikio hayo na kuwataka wasome kwa bidii ili hatimaye waweze kuongoza kitaifa na  Mkoa wa Dar es Salaam kwenye mitihani ya darasa la saba mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles