27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Hawa ‘wa Diamond’ afanyiwa upasuaji

Bethsheba Wambura, Dar es SalaamMsanii wa muziki wa Bongo Fleva Hawa Ramadhan maarufu Hawa Nitarejea, amefanyiwa upasuaji wa moyo katika hospitali moja iliyopo Bangalore nchini India, leo Jumatano Oktoba 24.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja wa msanii Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz, Hamis Tale maarufu Babu Tale, kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika upasuaji huo ulichukua saa tano na kusimamiwa na madaktari sita.

“Madaktari walichukua saa tano kumaliza kila kitu na kila kitu kimeenda vizuri,” ameandika Babu Tale.

Tale ambaye alisafiri na Hawa akiongozana na mama mzazi wa Hawa kuelekea nchini India mwishoni mwa wiki iliyopita, amesema tumbo la Hawa ambalo awali lilivimba kutokana na kujaa maji sasa limeshaanza kupungua na mgonjwa anaendelea vizuri.

Amesema Hawa alipofanyiwa uchunguzi iligundulika kinachomsumbua kwa asilimia 95 ni ugonjwa wa moyo na si ini kama alivyosema Hawa miezi miwili iliyopita alipofanyiwa mahojiano na Mtanzania Digital.

“Wataalamu walifanya vipimo na hawakuona tatizo linalohusiana na ini kwa mgonjwa ila ni moyo ndiyo uliokuwa unasababisha maji kujaa mwilini hivyo kutahitajika upasuaji mkubwa ambao utakua na uangalizi mkubwa wa wataalamu.

“Ahsante Mungu mgonjwa amemaliza salama na ameshazinduka na madaktari wametupa uhakika kuwa mgonjwa atakuwa salama na hadi hivi sasa tumbo limeshaanza kupungua na Mungu akipenda baada ya wiki moja na nusu ataruhusiwa kurudi Dar,” ameandika Tale.

Tale yuko India kwa niaba ya Diamond Platnumz ambaye amegharamia matibabu hayo baada ya kupata taarifa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa Hawa anaumwa na amewataka Watanzania waendelee kumuombea ili apate nguvu zaidi za kumsaidia na hatimaye arudi nchini salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles