26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Hatima ya Neymar kujulikana leo

PARIS, UFARANSA

HATIMA ya staa wa PSG, Neymar Jr, inatarajiwa kujulikana leo ambapo dirisha la usajili barani Ulaya litafungwa rasmi.

Mchezaji huyo raia wa nchini Brazil, amekuwa akitikiza vyombo vya habari duniani juu ya kutaka kuondoka katika klabu hiyo na kuhusishwa kuwindwa na timu yake ya zamani ya Barcelona na mabingwa wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid.

Neymar aliondoka Barcelona misimu miwili iliopita kwa uhamisho ambao ulitikisa dunia wa pauni milioni 198 ambayo haijawahi kuwekwa na mchezaji yeyote katika historia ya soka.

Usajili wa mchezaji huyo ndani ya PSG ulikuwa na lengo la kutakiwa kuisaidia timu huyo kutwaa mataji ikiwa pamoja na taji kubwa Ulaya la Ligi ya Mabingwa, lakini hadi sasa hajafanikiwa japokuwa bado ana mkataba wa miaka miwili mbele.

PSG waliweka wazi kuwa hawana mpango wa kuendelea na mchezaji huyo kutokana na tabia zake, hadi sasa hajapewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha PSG kwenye michezo ya msimu mpya wa ligi kwa madai anataka kuondoka.

Kuna taarifa kwamba viongozi wa timu ya Barcelona wapo nchini Ufaransa kwa ajili ya kuhakikisha dili hilo la kumrudisha mchezaji huyo kikosini mwao linakamilika kabla ya usiku wa leo kufungwa kwa dirisha la usajili Ulaya.

Jana kulikuwa na taarifa kwamba, mmoja kati ya mdhamini wa mchezaji huyo alitumia ukurasa wake wa Instagram na kuposti picha ya mchezaji huyo akiwa amevaa jezi mpya ya Barcelona, lakini alitumia dakika moja na kuifuta, ila tayari mashabiki mbalimbali waliiona na kuamua kuisambaza.

Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde, alipoulizwa juu ya kukamilika kwa dili hilo hakutaka kuweka wazi na badala yale alidai watu wasubiri kufungwa kwa dirisha la usajili Jumatatu ya leo ili mambo mengine yaendelee.

“Nasubiri kuona Jumatatu nini kitatokea kwa kuwa ndio siku ya mwisho ya usajili wa wachezaji Ulaya, ninaamini hapo ndipo itakuwa mwisho wa kelele za masuala ya usajili,” alisema kocha huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles