27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Hatima ya Kessy kutolewa ufafanuzi

kessy-640x5681-640x568_2

Na MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM

KAMATI ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji, wakati wowote inatarajia kutoa uamuzi kuhusu sakata la usajili wa beki, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, baada ya kupokea ripoti ya klabu za Simba na Yanga.

Kessy alisajiliwa na Yanga kwa ajili ya michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, lakini Simba iliwasilisha pingamizi ikidai kuwa wapinzani wao wamemsajili beki huyo bila kufuata taratibu.

Klabu ya Simba inadai kuwa Kessy alivunja mkataba kwa kuanza kufanya mazoezi na mahasimu wao Yanga pamoja na kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo kabla ya ule aliosaini akiwa kwa Wekundu wa Msimbazi kumalizika Juni 15, 2016.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, alisema kamati hiyo itakutana ndani ya siku mbili zijazo ili kutoa ufafanuzi wa ripoti hiyo kulingana na kanuni.

“Kamati ilizitaka klabu za Simba na Yanga kukutana ndani ya siku tatu ili kujadili suala la Kessy ili ziweze kufikiana makubalino na kutoa ripoti ambayo tayari wameiwasilisha,” alisema.

Lucas alisema kamati hiyo itachelewa kukutana kuipitia ripoti hiyo na kutoa uamuzi kwa kuwa viongozi na wajumbe wameajiriwa kwenye sekta nyingine tofauti na TFF, hivyo kubanwa na majukumu ya kikazi.

Awali kamati hiyo ilitarajia kutoa hukumu ya shauri la mchezaji Septemba 4 mwaka huu, lakini ikashindikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles