24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Hati fungani ya JASIRI ya NMB yashinda nishani ya Platnumz

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waandaaji wa Tuzo za Kimataifa za Mitaji kwa Wajasirimali wadogo na wa Kati kwa kushirikiana na Nchi za G20, Shirika la IFC (mwanachama wa Benki ya Dunia) pamoja na Jukwaa la Kufadhili Ujasiriamali (SME Finance Forum) mwaka huu wameanzisha kipengele kipya cha Hati Fungani Endelevu ya Mwaka kuzitunuku Taasisi zinazofanya vizuri kwenye eneo hilo.

Hati Fungani ya NMB JASIRI ndiyo imechaguliwa kama mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo mpya. Ushindi huo umepatikana baada ya Hati Fungani hiyo kupitiwa na jopo la majaji zaidi ya 100 waliovutiwa na mlengo wake, muundo na uwezo wa kulihudumia kifedha kundi ambalo halizingatiwi kwa Mitaji ya kawaida iliyozoeleka.

Chanzo hiki cha Mtaji kinaendana vyema na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na Kanuni za Dhamana za Kijamii za Chama cha Kimataifa cha Masoko ya Mitaji. Katika hotuba yake ya kukubali tuzo na heshima hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi Ruth Zaipuna, alisema:

“Sisi NMB tumejitolea kuhakikisha tasnia ya fedha inachangia maendeleo ya Tanzania. Hati Fungani ya JASIRI yenye lengo la kupunguza pengo la Mitaji linalozikabili biashara ndogo ndogo na za kati zinazomilikiwa au kusimamiwa na akinamama ni keielelezo kizuri cha dhamira hii,” amesema.

Hati Fungani yetu imefanikiwa kupata matokeo yaliyotarajiwa ya kusaidia kuwawezesha wanawake kiuchumi na kushughulikia madhumuni matatu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ambayo ni lengo la kwanza, la tano na la kumi.

“Tuzo hii ni wakati muafaka wa kihistoria kwa sekta ya benki nchini, kwani inaiweka nchi yetu katika ramani ya dunia kwa uongozi kwenye Mitaji endelevu. Hati Fungani ya JASIRI inaweka kigezo kipya nchini na barani Afrika katika kukuza vyanzo vingine vya Mitaji mbadala kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na wakimataifa,” alisema Zaipuna na kuongeza kuwa amesema tuzo hiyo ni kwa ajilia wa wafanyakazi wote wa NMB, washirika wake, wawekezaji na wasimamizi wa sekta ya fedha kwa kuchangia mafanikio makubwa ya dhamana ya JASIRI.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles