27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Hasunga apiga marufuku madalali wa mazao

Na MWANDISHI WETU-KYELA

WAZIRI wa Kilimo, Japhet Hasunga amepiga marufuku madalali wa mazao ya kilimo ambao wanatumia nafasi hiyo kuwagalaliza wakulima.

Agizo hilo alilitoa jana wilayani Kyela mkoani Mbeya, alipokuwa akizungumza mnada wa Kakao uliofanyika kwenye kijiji na kata ya Ikolo.

“Kumekuwa na wananchi wasiokuwa waaminifu kwa serikali na wakulima wake ambao wanawaibia wakulima maarufu kama Njemke, Butura, na Kangomba hivyo napiga marufuku biashara hiyo na endapo tukiwakamata tutawachukulia hatua za kisheria,” alisema Hasungas

Kutokana na hali hiyo amewaagiza wanunuzi hao wa Kakao na mazao mengine kuhakikisha kuwa wanawalipa wakulima fedha zao mara baada ya kukamilika kwa minada ili waweze kupata fursa ya kuandaa mashamba katika kipindi hiki cha msimu wa kilimo.

Alisema zao la Kakao litasalia kuuzwa kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani kwani kupitia mfumo huo ambao unasimamiwa chini ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakulima wataendelea kunufaika na mazao yao kwa kupata bei nzuri.

Alisema bado vyama vya ushirika vina matatizo makubwa lakini serikali itaendelea kusimamia kwa weledi vyama hivyo ikiwemo kuchukua hatua za haraka kwa viongozi wa vyama hivyo wanaotumia vibaya nafasi yao kwa kuwaibia wakulima.

“Kakao inayolimwa wilayani kyela nchini Tanzania ni miongoni mwa Kakao bora duniani ambayo ina ubora mzuri kuliko Kakao nyinyine zinazozalishwa katika nchi za Afrika Magharibi,” alisema 

Waziri Hasunga alishuhudia mnada wa Kakao katika Kijiji cha Ikolo ambapo imeuzwa kwa bei ya Sh 5,042 kwa kilo moja ambapo amesisitiza kuwa bei hiyo itakuwa na manufaa makubwa kwa wakulima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles