30.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Harmonizer: Diamond hana dharau

DSC_0266NA CHRISTOPHER MSEKENA

MKALI wa ngoma ya ‘Aiyola’ Rajabu Abdulkhali maarufu kama Harmonizer amesema kuwa bosi wake Diamond Platnumz hana mashauzi na dharau kama wengi wanavyomfikiria.

Akibonga na Swaggaz juzi jijini Dar es Salaam, Harmonizer alisema kuwa tuhuma hizo zinatokana na namna nyota huyo wa wimbo wa Nana anavyojiweka, lakini ni mtu poa sana ndiyo maana alikubali kumsaidia na kumsimamia vyema kimuziki.

“Diamond angekuwa na dharau asingenisaidia kufika hapa nilipo, ni mtu poa sana, anapenda kumsikiliza kila mtu lakini labda mwonekano wake kwa jamii ndiyo unafanya wengi wafikiri labda ana mashauzi,” alisema.

Harmonizer ni msanii wa kwanza kutoka kwenye Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) inayomilikiwa na Diamond Platnumz, mshindi wa tuzo tatu za AFRIMMA mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,212FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles