28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Harmonize mguu ndani mguu nje WCB?

SWAGGAZ RIPOTA

AGIZO la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhusu kuchunguzwa kwa nyota wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’, kama anatumia bangi au laa ili aweze kukamatwa, limenifikirisha vitu vingi na kufanya nianze kutazama kwa ukaribu mwenendo wa hivi karibuni wa memba huyo wa WCB.

Licha ya mazuri mengi ambayo amekuwa akiyafanya kama vile kusaidia walemavu, kutoa mitaji kwa wanawake na vijana wajasiliamali, kufanya shoo kubwa zinazoacha gumzo pamoja na kuzidi kupaa kimuziki, Harmonize amekuwa tofauti kitabia na yule wa kipindi kile anaatoka.

Ukitazama ukurasa wake wa picha ambao mpaka sasa una wafuasi zaidi ya milioni 2.9, utagundua mambo kadhaa ambayo hapo awali hakuwanayo. Mengi ni mabaya yanayofunika mazuri, jambo linalowaumiza wanaopenda mafanikio yake.

TABIA YA KUVUTA SIGARA

Katika agizo la mlezi wa WCB, Paul Makonda alilolitoa juzi katika kikao chake na wasanii, alisema tabia ya ajabu ni miongoni mwa sababu zinazokwamisha wasanii wengi kupata dili kwa kuwa kampuni nyingi zinataka mtu safi asiye na uchafu mbele ya jamii.

Ndiyo maana akiwa kama baba wa WCB, alimwomba gavana wa Accra, Ghana amchunguze kijana wake Harmonize kama anachovuta hadharani ni sigara au bangi ili kama ni dawa za kulevya basi akitua Bongo, aweze kuwekwa rumande na kufunguliwa kesi kama ile ambayo ilimkuta mrembo Wema Sepetu.

Hiyo yote imetokana na tabia mpya ya staa huyo, kuvuta sigara hadharani jambo ambalo ni hatari kwa jamii ya vijana wadogo wanaomtazama kama kioo pia hata kwa afya yake akiwa kama msanii wa muziki anayeiwakilisha vyema Tanzania huko ulimwenguni.

MGUU NDANI MGUU NJE WCB?

Harmonize kwa sasa ni msanii mkubwa. Ukitazama msafara wake wenye walinzi mbavu nene wapatao wanne utagundua jamaa siyo wa mchezo na tayari ameanza kujijengea ‘empire’ au utawala wake akiwa bado ni memba wa WCB.

Licha ya mambo kadhaa yanaonyesha, Harmonize bado ni msanii wa WCB, kuna tetesi zilizotokana na mwenendo wa msanii huyo na  viongozi wa WCB kuwa kwa sasa Konde Boy, mguu mmoja ndani na mwingine upo nje ya lebo hiyo kubwa Afrika.

DIAMOND ASHANGILIA AGIZO LA MAKONDA

Wakati Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, akitoa kauli ya Harmonize kushughulikiwa kutokana na tabia yake ya kuvuta hadharani kitu kinachotoa moshi unaofanana na bangi, Diamond Platnumz alionekana akipiga makofi.

Hiyo ni ishara kuwa anapongeza na amefurahishwa na agizo hilo ambalo kama ni kweli linakwenda kumtia matatani Harmonize ambaye ni msanii wake.

SAPOTI IMEKUWA NDOGO

Tetesi zimeendelea kudai kuwa huwenda Harmonize hayupo sawa na Diamond Platnumz au viongozi wake kutokana na sapoti ndogo ambayo amekuwa akipewa hivi karibuni tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.

Mfano wimbo Paranawe wa Harmonize aliofanya na Rayvanny, Diamond Platnumz, hakuwahi kuuposti katika ukurasa wake wa Instagram kama ilivyokawaida yao kusapotiana. Hata mameneja wao kama Sallam Sk, Babu Tale na Mkubwa Fella hawakuupa sapoti mtandaoni wimbo huo kama ambavyo wanawapa kina Rayvanny, Mbosso, Lavalava na wasanii wengine.

Hali kadharika hivi karibuni Harmonize, anaachia albamu yake fupi (EP) inayoitwa Afro Bongo. Hii ni albamu kubwa inayotarajia kusumbua chati mbalimbali za muziki Afrika akiwa ameshirikiana na staa wa Nigeria, Burna Boy.

Jambo la kusangaza, Harmonize amekuwa akiipa promo yeye mwenyewe bila sapoti ile kubwa ambayo tumezoea kuioa WCB wakipeana.

HARMONIZE ANAKWAMA WAPI?

Hakuna anayeweza kubisha kuwa Harmonize ni msanii bora zaidi kwa sasa, tazama nyimbo zake zinavyoweka rekodi kubwa, fuatilia shoo zake anazofanya, utagundua ni msanii ambaye atadumu kwa muda mrefu kwenye muziki.

Harmonize, anakwama pale ambapo anaanza kulewa sifa kipindi hiki ambacho Afrika imempokea vizuri na tayari ameanza kuuwakilisha vyema ukanda huu wa Afrika Mashariki kama mwenyewe anavyojiita ‘East African Young Star’.

Anaweza asione mapungufu hayo lakini ni vizuri akasikia kelele za mashabiki wanaompenda, wakimuonya kuwa siyo vizuri kwa afya yake kutumia moshi, siyo jambo jema  kujikweza ila vizuri kujilinda, kuwekekeza kwenye kazi na kusaidia jamii ili aendelee kudumu miaka na miaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles