26.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

DC Busega: Mimba kwa wanafunzi 90 ni hatari, siwezi kuvumilia

Derick Milton, Busega.

Mkuu wa Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Tano Mwera amesema atahakikisha hatua za kisheria na hukumu zinatolewa kwa kupata ushahidi unaotakiwa kwa wote watakaojaza mimba wanafunzi katika wilaya yake ya Busega.

Kauli hiyo amewaeleza wazazi na wanafunzi wa kike 300 wa shule za sekondari Lamadi, Mkula pamoja na Nyangwe, alipozungumza nao Februari 1 wakati wa kampeini yake ya Binti Itambue Thamani Yako inayolenga kupiga vita mimba na ndoa za utotoni Wilayani humo.

Mwera amesema Wilaya hiyo kwa mwaka 2018 jumla ya wanafunzi 90 wa kike shule za msingi na sekondari wamepata mimba wakiwa shuleni huku kesi nyingi za watoto hao zikishindwa kufikia hatua ya hukumu kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha.

Kiongozi huyo amesema kuwa watoto 90 kupata mimba ni wengi sana, na yeye kama kiongozi wa Wilaya hawezi kuvumilia hali hiyo badala yake atapambana kuhakikisha wahusika wote wanachukuliwa hatua za kisheria.

“Bado kuna wazazi wanawalazimisha watoto wa shule waolewe, niwaombe wanafunzi wa kike kama kuna dalili hizo nyumbani kwenu toeni taarifa kwangu haraka ili nichukua hatua,” amesema.

Awali akiongea katika kampeini hiyo Mratibu wa vijana kutoka Chama cha Wanawake Wakristo Tanzania (YWCA), Rose Manumba, amewataka wanafunzi hao watumie nafasi kielimu ili wafikie malengo yao.

“Tumieni hii nafasi ya elimu vizuri ni muhimu sana kufikia malengo yenu, msikubali kuyumbishwa, kataeni makundi ya marafiki wabaya,” amefafanua Manumba.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,509FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles