Bethsheba Wambura, Dar es Salaam
Msanii wa Bongo fleva Rajab Kahali maarufu Harmonise ametangaza nia ya kumsaidia msanii mwenzie Aboubakary Katwila maarufu Q Chilla ili kumrudisha tena kwenye soko la muziki baada ya kupotea kwa miaka kadhaa na
Harmonize amesema kwa kuanzia watatoa EP (albam fupi) yenye nyimbo tatu na video zake ambazo wameshirikiana kwa pamoja na wameipa jina la ‘Return of Q Chilla’ na itaachiwa leo Jumatatu Julai 22, .
Akizungumza na waandishi wa habari leo jumatatu Julai 22, Harmonise amesema anamsaidia Q Chilla kwa kushirikiana na uongozi wa lebo ya WCB chini ya msanii Nasib Abdul maarufu Diamond Platnumz.
“Q Chilla ni msanii mkubwa hapa nchini na ndiyo chanzo cha maendeleo ya muziki wetu kwa kushirikina na uongozi wa Wasafi tumeona tushirikane na watanzania kuhakikisha kipaji chake hakipotei ili pia apate maisha mazuri na familia yake,” amesema Harmonize.
Aidha Harmonize amesema yeye na uongozi wake wamejichanga na kumnunulia gari aina ya Toyota Porte ili kumsaidia katika usafiri kwani Q Chief ni msanii mkubwa si vyema akaendelea kutumia pikipiki na usafiri mwingine wa kukodi.
Kwa upande wake baada ya kupewa zawadi hiyo Q Chilla alimshukuru Hamonize pamoja na uongozi wake kwa kumjali na kumuonyesha upendo wa pekee.
“Najiuliza huu upendo ni wa aina gani nitaulipa vipi niwashukuru kwa moyo walio uonyesha naahidi kuto waangusha katika ujio wangu huu mpya,” amesema Q Chilla.