SIRI ya baba halisi wa mtoto wa pili wa mwanamitindo, Hamisa Mobetto imefichuka baada ya mrembo huyo kubadilisha jina la awali la ukurasa (Instagram) wa mtoto wake huyo wa kiume na kuweka lingine linaloshabiiana na la staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Diamond Platnumz ambaye ni baba wa watoto wawili, Tiffah na Nillan aliyezaa na raia za Uganda mrembo, Zari amekuwa kwenye skendo ya kuchepuka na Hamisa Mobetto kuanzia mwaka jana wakati wa uandaaji wa video ya wimbo wa Salome licha ya msanii huyo kukataa.
Viashiria vya Hamisa kupata mtoto na Diamond Platnumz vimeendelea kujidhihirisha baada ya familia ya staa huyo wa singo ya Eneka yaani mama mzazi na dada yake kuonekana wakitoka hospitali kumtazama Mobetto na mtoto wake huyo ambaye Agosti 8 mwaka huu alimfungulia ukurasa wa Instagram na kumuita Tanzanian Baby.
Katika kile kinachoonekana Hamisa amechoka kuficha siri hiyo, Jumatano wiki hii mrembo huyo alibadilisha jina la ukurasa wa mtoto wake kutoka Tanzanian Baby mpaka Abdul Naseeb au Prince Dully Dee, kitu kilichoonyesha wazi kuwa baba halisi wa mtoto huyo ni Daimond Platnumz ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul.
Katika hali ya kuoenakana kukanusha taarifa hizo na kusema Hamisa Mobetto anatafuta umaarufu, Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika: BITCH IS DYING FOR FAME!!.