27.4 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yazindua Promosheni ya “Shinda na Halopesa”

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya huduma za Mawasiliano ya mkononi nchini ya Halotel Tanzania kupitia mfumo wake wa kifedha wa Halo Pesa imewahumiza wateja wake kuendelea kutumia huduma za kifedha kwa njia ya simu ili kujinyakulia zawadi mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na jijini Dar es Salaam leo Machi 28, katika uzinduzi wa promosheni ya SHINDA NA HALOPESA, ambayo inatoa fursa mbalimbali kwa wateja wake kujishindia zawadi za fedha taslimu na pikipiki maarufu kama Shinda na Bodaboda.

Naibu Mkuu Mkurugenzi wa HaloPesa, Magesa Wandwi, amesema wanafurahia wakati wote kuwa katika tasnia ya utoaji wa huduma za Kifedha Kidigital ambazo zinawapa wateja wao fursa ya kufanya miamala kwa njia ya simu.

“Tumekuja na Promosheni hii ya SHIDA na HALOPESA ili kuendelea kutia chachu kwa wateja wetu na watanzania ili waendelee kutumia huduma za Kifedha za HaloPesa ikiwa ni katika malengo thabiti na ajenda ya Serikali kwa ujumla kuwafanya watanzania wengi kutumia mifumo ya kifedha,” amesema Mages.

Kwa Upande wa Afisa Masoko wa HaloPesa, Roxana Kadio, amesema kuwa Promosheni hiyo itakayoendeshwa kwa muda wa wiki nane ni maalumu kwa wateja wa HaloPesa, ambapo jumla ya wateja 72 watajishindia zawadi mbalimbali, wateja 64 watajishindia zawadi ya fedha taslimu zitakazotolewa kila siku kwa kipindi cha miezi miwili, wapo watakaojishindia fedha taslimu Sh 50,000 na wengine Sh 100,000 kila siku.  Aidha wateja 8 watashinda pikipiki mpya kila wiki kwa kipindi cha mieizi miwili.

“Ikiwa huduma hii inakuwa kwa haraka zaidi, Halopesa imesambaa na kuendelea kote nchini kwa kutoa huduma mbalimbali za kifedha zenye ubunifu na rahis kutumia kwa gharama nafuu ambapo itasaidia watanzania wengi kujikwamua,” amesema Kadio.

Aidha, amesema Halotel inaendelea kuwahimiza wateja wake na wale ambao hawajaanza kutumia huduma ya HaloPesa kuchangamkia Promosheni hii kwa kufanya miamala mingi iwezekanavyo ili kujiongezea nafasi ya kushinda na kujipatia zawadi mbalimbali za fedha taslimu na Bodaoda 

Ameongeza kuwa HaloPesa ni chaguo la wateja na Halotel inafurahi zaidi kuwapatia huduma hii bora, Rahisi na zenye gharama nafuu ambapo HaloPesa  ni familia “HaloPesa ni Maisha ishi nayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles