24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yatoa Tbasamu kwa Yatima kuelekea Sikukuu ya Idd

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kwa kushirikiana na Jamii ya Tanzania imetoa Msaada kwa Kituo cha watoto Yatima kiitwacho Fadhillah Orphanage Center kilichopo Misugusugu mkoani Pwani, katika kuboresha, kuonesha upendo na kuwaletea tabasamu watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Aidha, kampuni hiyo imetoa msaada wa vyakula, mbuzi na mahitaji mengine ya muhimu kwa watoto wa kituo hicho, ikiwa ni mkono wa sikukuu ya Eid Mubarak.

Akizungumza leo Aprili 20, 2023 wakati wa kukabidhi Msaada huo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Halotel, Sakina Makabu amesema kuwa Msaada huo ni Utaratibu wa Kampuni ya simu ya Halotel kuikumbuka Jamii hasa watu walioko katika mazingira magumu.

“Mbali na kampuni kutoa msaada huo, Halotel imezielekeza ofisi zake zilizoko Mikoa mbalimbali nchini kusaidia makundi mbalimbali kama ilivyofanya mkoani Pwani,”alisema Sakina.

Kituo hicho cha Fadhillah Orphanage Center kinalea watoto 168 ambao ni Yatima waliopoteza wazazi wao, huku watoto wengi wao walipitia changamoto nyingi na kinatoa mazingira salama na upendo na kupata huduma na msaada wanaohitaji.

“Leo tunatoa mifuko ya kilo 150 ya mchele, kilo 50 za maharage, ndoo za lita 80 za mafuta ya kupikia, kilo 100 za unga wa mahindi, kilo 50 za sukari, tambi mifuko 100, mbuzi wawili, sabuni za usafi wa mwili na kufulia, pampas za watoto pamoja na vifaa kwa ajili ya shule huku zawadi hizi zote ikiwa ni kwa ajili ya kutoa tabasamu na mkono wa Sikukuu ya Eid Mubarak,” amesema Sakina.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Kituo hicho, Sureiya Shehe, ametoa Shukrani kwa Kampuni ya Halotel, kwa upendo na utu wa kujali waliouonesha kwa kukumbuka watu wanaoishi katika mazingira magumu.

“Tunashukuru kwa mchango huu, ambao utaleta tofauti kubwa kwa watoto hawa ambao wanahitaji mahitaji ya msingi kama chakula na vifaa vya shule na zaidi ikiwa ni kuwa fanya watoto wetu kuweza kufurahia sikukuu kama watoto wengine. Tunathamini jitihada hizi za Halotel kusaidia jamii yetu na tunatarajia waendelee kufanya hivi hata mikoa mingine ili waweze kuboresha maisha ya Watanzania,” amesema Sureiya.

Aidha, msaada wa Halotel kwa kituo hiki ni moja ya utaratibu ambao utaendelea kutekelezwa mara kwa mara ili kujenga mahusiano mema na jamii ambayo pia ni wateja na Watanzania kwa ujumla, ambapo Utaratibu huo unatekelezwa kufuatia sera bora ya Kampuni hiyo kupitia Program za kurudisha kwa jamii mbali na kutoa huduma bora za mawasiliano nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles