23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yabadili nembo yake, yaahidi huduma bora

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Katika kuboresha huduma zake za interneti nchini, kampuni ya ya Mawasiliano ya Halotel imedhamiria kufanya maboresho zaidi katika kupanua wigo kwa wateja wake kwa kubadili nembo yake ili kuendana na huduma stahiki. 

Nembo mpya ya Halotel inaendelea kudumisha rangi ya Machungwa ya kampuni.

Hata hivyo, muonekano wake umeboreshwa ili kuonesha maendeleo na dhamira ya kuboresha zaidi huduma katika sekta ya mawasiliano nchini.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Abdallah Salum wakati wa maonyesho ya kimataifa ya biashara ya 47 yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Salum alisema kuwa kubadilika kwa nembo hiyo ya Halotel ni moja ya maboresho ya kampuni hiyo kwenye huduma zake mbalimbali ikiwemo huduma za intaneti kwenda 4G nchi nzima ikiwa ni dhamira ya kuwapa wateja wetu na watanzania kwa ujumla suluhisho za huduma bora na za kidigitali kulingana na mahitaji yao Kimawasiliano popote walipo.

Salum alisema kuwa katika msimu huu wa maonyesho ya Saba Saba pia wanaendelea kutoa offer mbalimbali kwa wateja wao wa awali na wapya watakaojisaliji na mtandao wa Halotel na wale wanaobadili laini zao kwenda 4G.

“Moja ya maboresho yetu kwa sasa ni kubadilisha logo yetu na kuwa na muonekano unaoendana na huduma zetu mpya zilizoboreshwa zaidi. Wateja wetu sasa wa wataweza kupata huduma zetu za 4G za intanet bila vikwazo,” amesema Salum na kuongeza kuwa:

“Mabadiliko haya ya logo yanaenda sambamba ya kauli mbiu yetu Mpya ‘Pamoja kwa Ubora’ ni sehemu ya mikakati ya ukuaji na kuboresha kampuni ya Halotel. Tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora zaidi za mawasiliano na za teknolojia kwa wateja wetu, kwa kuzingatia mahitaji ya soko la kisasa katika sekta ya Mawasiliano nchini Tanzania,” ameongeza Salum.

Baadhi ya ofa ambazo Halotel wanaendelea kutoa kwa wateja wake wapya na wanaobadilisha  laini zao simu kwenda 4G katika msimu huu wa maonesho na sikukuu ya Sabasaba ni pamoja na Simu janja za mkononi mpya kabisa aina ya Sumsung Galaxy A 14, muda wa maongezi, t-shirts, vikombe keyholder na kofia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles