25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Halmashauri ya Mji Mafinga yapewa heko kwa kupata hati safi

Na Raymond Minja, Iringa

Halmashauri ya Mji Mafinga imepewa heko kwa kupata hati safi
miaka sita mfululizo kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hatua ambayo imeendelea kuupatia safa Mkoa wa Iringa.

Akizungumza juzi katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitia hoja za CAG, Mkuu wa Moa wa Iringa, Queen Sendiga amesema kutokana na kufanyakazi kwa ushirikiano
umepelekea halmashauri hiyo kupata hati safi.

Sendiga amesema kuwa Baraza la halmashauri hiyo limekuwa likifanya kazi vema na kwa ushirikiano jambo ambalo limekuwa mfano wa kuigwa na halmashauri nyingineza mkoa huo.

“Pamoja na mafaniko haya, niwatake watumishi wa halmashauri hii kuendelea
kufanya kazi kwa kujituma kulingana na maeneo ambayo mnayafanyia kazi.

“Pia nimuagize Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Mafinga kuwachukulia hatua za kisheria watumishi wazembe kazini ambao wamekuwa wakisababisha hoja za CAG,” amesema Sendiga na kuongeza kuwa:

“Haiwezekani kila wakati mtumishi anakuwa anasababisha hoja za CAG na hachukuliwi hatua yoyote na anaendelea kufanya kazi hapo hapo bila kuwajibishwa,” amesema Sendiga.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa, zilipatikana hoja 30 za CAG ambapo jumla ya hoja 13 zimefanyiwa kazi na 17 bado hazijafanyiwa kazi, hivyo amegiza hoja hizo zifanyiwe kazi haraka iwezekavyo.

Sendiga amesema kuwa baadhi ya watumishi ambao wanahusika
kukusanya mapato wamekuwa sio waamifu kwa kuwa wamekuwa wanazima mashine za
kukusanyia mapato jambo ambalo ni ubadhilifu wa fedha za serekali.

“Haiwezekani mashine inazimwa kwa zaidi ya siku 1,000
haifanyi kazi na viongozi mpo hapo haiwezekani kabisa nakwambia Mkurugenzi
wachukuliwe hatua kali watumishi wanaosababisha kupotea kwa mapato ya
halmashauri,” amesema Sendiga.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule alisema
kuwa wanafanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato, ushirikiano mzuri, wanatoa
mikopo, wanafanya vizuri kwenye uchumi kutokana na kufanya kazi kwa
ushirikiano.

Mtambule amesema kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga
amekuwa kiunganishi kikubwa baina ya wakuu idara na wafanyakazi wengine wa
halmashauri kuwa kitu kimoja katika kufanya kazi.

Almesema kuwa ukatilii wa kijinsia bado upo wilaya ya
Mufindi lakini wamekuwa wakitoa elimu mara kwa mara ili kuhakikisha wananchi
wanajua madhara ya ukatili wa kijinsia na kupinga vitendo vyote ya ukatili.

Nae Mkurugenzi wa halmashauri ya Mafinga Mji, Happiness Laizer amesema kuwa wameyapokea maagizo yote ya Mkuu wa Mkoa juu ya hoja za CAG nakwamba watayafanyia kazi ili kuhakikisha hawapati hojanyingine mpya huku wakijitahidi kuzijibu na kuzimaliza hoja zote za CAG.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles