25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri Bukoba yapitisha Bilioni 42.7

Renatha Kipaka, Bukoba

Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera limepitisha bajeti ya zaidi ya Sh bilioni 42.7 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Akisoma mapendekezo ya mpango huo wa bajeti juzi Jana kwa mwaka huo wa fedha, Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Manase Mollel amesema kuwa zaidi ya Sh bilioni 32.3 ni ruzuku ya mishahara na kwamba ruzuku ya matumizi ya kawaida ni zaidi ya Sh bilioni 1.5,.

Amesema miradi ya maendeleo ni zaidi ya Sh bilioni 6.6 na mapato ya ndani ni zaidi ya Sh bilioni 2.2.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani chakupitisha bajeti hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Murshid Ngeze ametaja vipaumbele vya bajeti hiyo kuwa ni utoaji wa mikopo asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na ukamilishaji wa hospitali ya wilaya iliyopo eneo la Bujunangoma.

Ngeze ambae pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania –ALAT- Taifa ametaja vipaumbele vingine kuwa ni ukamilishaji wa ujenzi wa Stendi ya mabasi na maroli ya Kemondo, ujenzi wa fremu za biashara katika eneo la kwa Kagambo jirani na ofisi ya maji- RUWASA na kuboresha huduma za afya.

“Vipaumbele vingine ni kusimamia usafi wa mazingira, kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi msingi na sekondari, kupunguza udumavu kwa watoto, kuimarisha huduma za uganii na kuboresha motisha ya wafanyakazi,” amesema Ngeze.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles