25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

‘HALI YA VYOMBO NCHINI VYA HABARI NI MBAYA’

Na ASHA BANI – Dar es Salaam

BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limesema haliridhishwi na hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini kwa sasa.

Limesema hadi sasa kuna matukio 120 ya waandishi kupigwa na kunyanyaswa, ufungiaji wa magazeti, kutishwa na kunyimwa taarifa, kutekwa na kuuawa tangu mwaka 2012 hadi kufikia jana.

MCT imesema kufungwa kwa magazeti matano mfululizo katika   muda mfupi kimedhihirisha kwamba hali si shwari.

Magazeti hayo ni Mseto, Mwanahalisi, Mawio, Tanzania Daima na RAIA Mwema.

Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alikuwa akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya  mataifa ya kupinga jinai dhidi ya wanahabari Dar es Salaam jana.

Alisema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini si nzuri kutokana na kuendelea kwa madhira siku hadi siku.

Mukajanga alisema katika   miaka miwili iliyopita hofu kwa waandishi wa habari na tasnia nzima imekuwa ikiongezeka na kusababisha kutofanya kazi zao kwa uhuru na weledi.

Alisema mbali na vyombo vya habari kufungiwa, waandishi wamepata misukosuko wakiwa kazini.

“Baadhi yao ni pamoja na Halfani Liundi wa ITV Arusha ambaye aliwekwa kizuizini na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.

“Waandishi wengine waliopatwa na madhira ni    Augusta Njoji  wa Nipashe ambaye hivi karibuni aliandika habari za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) lakini alikamatwa na polisi na baadaye kuachiwa kwa dhamana.

Katibu Mkuu huyo wa MCT alitaja vyombo vingine ambavyo waandishi wake wamepata misukosuko ya vyombo vya dola wakiwa kazini kuwa ni   Mwananchi, Azam TV na MTANZANIA.

“Ukiukwaji mkubwa wa uhuru wa waandishi wa habari umekuwa ni serikali kupitia polisi, wakuu wa mikoa, wilaya ukiachia wizara ambayo baadhi ya magazeti yalifungiwa yanalalamika mahakamani.

“MCT tunasisitiza kuwa hali ya kupata habari na uhuru wa kujieleza ni haki ya mtu binafsi na vile vile haki ya jamii.

“Hali hii na uhuru vinawekwa wazi na kulindwa na katiba za nchi za Afrika na matamko mbalimbali ya kimataifa na kikanda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles