26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Hailey amtaka Bieber kumpa mtoto

LOS ANGELES, MAREKANI



MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Hailey Baldwin, ameweka wazi kuwa amemtaka mpenzi wake, Justin Bieber, kumpa mtoto haraka iwezekanavyo.

Wawili hao waliweka wazi kuwa wanatarajia kufunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu, lakini mwezi mmoja uliopita kulisambaa taarifa kwamba tayari mastaa hao wamefunga ndoa ya kimya kimya.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22, ameweka wazi kuwa anataka kupata mtoto muda wowote kuanzia sasa kutoka kwa mpenzi wake huyo.

“Ninapenda sana watoto, hivyo sitaki kusubiri kuwa na watoto wangu, ninasema hayo sasa na nadhani jambo hilo linakaribia kutoka kwa mpenzi wangu Bieber,” alisema mrembo huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles