RAIS wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), Javier Tebas, amesema klabu ya Real Madrid itamudu kuwanunua Kylian Mbappe na Erling Braut Haaland bila kuvunja kanuni ya Kanuni ya Nidhamu ya Utumizi wa Fedha (Financial Fair Play).
Awali, zilikuwapo taarifa zinazodai Madrid itavunja kanuni hiyo endapo itawanasa wawili hao kwa mpigo wakati wa usajili wa kiangazi hapo mwakani.
“Madrid wameuza wachezaji wenye thamani ya euro milioni 200,” amesema Tebas na kuongeza: “Wana mkwanja wa kutosha wa kuwasajili Mbappe na Haaland. Hawajapoteza fedha…”
Kauli yake hiyo inatafsiriwa kuwa ni juhudi za kurejesha heshima ya La Liga baada ya Ligi Kuu hiyo kuonekana kupoteza mvuto baada ya kumpoteza Lionel Messi aliyeondoka Barcelona na kutimkia PSG.