27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

GUTERRES ATETEA MAKUBALIANO YA NYUKLIA YA IRAN

UN, NEW YORK


KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres ameionya Marekani dhidi ya kuyafuta makubaliano ya kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran bila kuwepo njia nyingine bora ya kusuluhisha mzozo huo.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) hapo jana, Guterres alisema makubaliano hayo yaliyofikiwa baina ya Iran na nchi zenye ushawishi mkubwa duniani yalikuwa ni ushindi wa kidiplomasia, na kuongeza ingekuwa busara kuyaendeleza.

Hata hivyo, alipendekeza mjadala kuhusu tofauti zilizopo, akisema anaamini ukanda wa Mashariki ya Kati uko katika hali ya mashaka makubwa.

Akirejea kuhusu wasiwasi wa baadhi ya nchi juu ya kupanuka kwa ushawishi wa Iran katika ukanda huo, Guterres alisema hilo halipaswi kuhusishwa na makubaliano juu ya mpango wa nyuklia.

Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akitishia kuyafuta makubaliano hayo, tofauti na nchi nyingine wadau ambazo zinataka yabaki kama yalivyo.

Viongozi wa Ulaya wamemtaka pia Rais Donald Trump wa Marekani kubakia katika makubaliano hayo.

Trump amekuwa akiyaita makubaliano hayo-mkataba mbaya zaidi na kuonesha nia ya kutaka kujitoa, uamuzi ambao atautoa siku chache zijazo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles