27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

GUARDIOLA: TIMU 48 KOMBE LA DUNIA LITAUA WACHEZAJI

Pep Guardiola
Pep Guardiola

MANCHESTER, ENGLAND

BAADA ya Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), Gianni Infantino, kutoa wazo la kuongezeka kwa timu kufikia 48 badala ya 32 katika michuano ya Kombe la Dunia, kocha wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, amedai kuwa mfumo huo utaua wachezaji.

Guardiola amedai kuwa mfumo huo utawafanya wachezaji kucheza soka kwa muda mrefu katika michuano hiyo na kuufanya muda kuwa mfupi wa maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu kwa klabu mbalimbali kwa kuwa wachezaji wao watakuwa katika timu za taifa.

Mwanzoni mwa wiki hii Rais wa Fifa, Infantino, aliweka wazi kuwa timu ambazo zinashiriki michuano ya Kombe la Dunia zinatakiwa kuongezeka badala ya kuwa 32 na sasa zinatakiwa kuwa 48, huku katika michuano ya Euro inatakiwa kuwa na timu 24 badala ya 16.

Kutokana na kauli hiyo ya rais wa soka la kimataifa, kocha wa Man City, Guardiola, ameonekana kupingana nayo na kudai kuwa kama ni hivyo basi ni bora timu zikapewa nafasi ya kubadilisha wachezaji zaidi ya watatu.

“Hii si kwa ajili ya soka la nchini England peke yake, ni kwa soka duniani kote, kwa sasa tunazungumzia habari ya michuano ya Kombe la Dunia ambapo timu zinatakiwa kuongezwa hadi kufikia 48, ninaamini hii itakwenda kuua wachezaji wetu.

“Tunakwenda kuangalia ubora na tunasahau wingi wa timu, hii itapelekea wachezaji kukosa muda wa kutosha kupumzika, watakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kuwa na michezo mingi katika michuano hiyo.

“Nchini Hispania kuna timu nne ambazo zinashiriki Klabu Bingwa UIaya, huku timu tatu zikiwa zinashiriki Europa Ligi, kutokana na hali hiyo timu za Hispania zitakuwa zinasonga mbele mara kwa mara zaidi ya England.

“Tunakubaliana na maamuzi ambayo yametolewa na Rais wa Fifa na kama tutakuwa hatuna furaha na maamuzi hayo basi tutarudi nyumbani lakini ukweli ni kwamba tutapoteza ubora wa wachezaji wetu.

“Hii nimefikiria kwa wachezaji ambao wanapumua, wanahitaji kupumzika pamoja na kufurahia maisha yao, lakini aina hii ya soka ninaamini ni ngumu, kwa kuwa tunakwenda kumaliza msimu na mara baada ya wiki moja Kombe la Dunia linaanza na mara baada ya kumalizika wiki tatu mbele timu zinaanza maandalizi ya ligi nchini China, United States, Australia.

“Baada ya hapo kuna michuano ya Euro, inaweza kufanyika hivi kwa miaka 10 au 12, lakini hatuwafikirii wachezajiwetu, kutokana na hali hii klabu inatakiwa kuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya matumizi. Tunabadilisha wachezaji watatu katika kikosi na kwanini isiwe wachezaji wanne, tano au sita? Tunatakiwa kuwatetea wachezaji wetu,” alisema Guardiola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles