28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

GGML yaongeza udhamini kwa Geita Gold FC msimu wa 2022/2023

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeongeza mkataba wa udhamini kwa Klabu ya Geita Gold Football Club (GGFC) wenye thamani ya  Sh milioni 800 kuanzia tarehe 16 Desemba 2022.

GGML ilipata haki ya kipekee kama wadhamini wakuu wa Klabu kwa mechi na matukio yote yanayohusiana na Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2022-2023 (NBC Premier League) kwa mujibu wa makubaliano hayo.

Katika msimu wa 2020/21, Klabu ya Geita Gold FC ilitimiza malengo kadhaa ikiwa ni pamoja na kushiriki katika mechi za kimataifa.

Geita Gold, iliyokuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ilipata mafanikio hayo kwa mara ya kwanza baada ya kushika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya NBC msimu uliopita.

Katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika hivi karibuni kwenye Makao makuu ya Halmashauri ya Mji wa Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong alisema kuwa makubaliano hayo yameifanya GGML kuwa wadhamini wakuu wa klabu ya Geita Gold Football Club.

“Msimu uliopita, GGML ilikubali kudhamini klabu ya Geita Gold Football Club kwa Sh milioni 500; hata hivyo, kwa mwaka 2022, udhamini wetu umeongezwa hadi Sh milioni 800.

“Kama ilivyotajwa kwenye MOU, GGML ingependelea udhamini huu kuwezesha ununuzi wa basi la Klabu, milo ya timu na vifaa vya michezo. Tunatarajia udhamini wetu utarahisisha ushiriki wa timu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2022-2023, pamoja na shughuli nyingine za klabu,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya utiaji saini alifurahishwa kuona pande hizo mbili zikitia saini makubaliano hayo kwa kuwa yatakuwa na ushawishi chanya mkoani Geita.

“Geita Gold Football Club ni kielelezo cha sifa chanya za mkoa wa Geita. Timu imefanikiwa kutambulisha wilaya na mkoa wetu. Kwa sasa kila mtu anafahamu eneo la kijiografia ya mkoa wetu,” alisema na kuzitaka pande hizo mbili kufikiria kuunda Chuo cha michezo mkoani Geita ili kuibua vipaji vya vijana.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Zahara Michuzi, alipongeza GGML kwa kuwa na moyo wa kujitolea kwa ajili ya klabu ya Geita Gold FC.

“Ufadhili huu wa GGML katika klabu hii umekuwa na matokeo chanya. Shauku na juhudi za wachezaji ni matokeo ya uwekezaji wa GGML. Tunashukuru kwa dhati kutokana na msaada huu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles