29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

GGML watumia Bilioni 1 kusimika mtambo wakuchenjua makinikia

*Ni mtambo pekee Afrika Mashariki, Kati, unalindamazingira

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katika kutekeleza mpango wa kulinda mazingirapamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025, Kampuniya Geita Gold Mining Limited (GGML) imenunua nakusimika mtambo wenye thamani ya Sh bilioni moja kwa ajili ya kuchenjua kaboni ‘makinikia’ yanayotokanana shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu.

Mtambo wa uchenjuaji kaboni maarufu kama makinikia ulionunuliwa na kusimikwa mkoani Geita kwa thamani ya Sh bilioni moja na Kampuni ya GGML. Mtambo huo wa kwanza Tanzania, Afrika mashariki na kati utawezesha serikali kuongeza mapato pamoja na ajira katika sekta ya madini.

Hatua hiyo inaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza napekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuwana mtambo huo kwani hapo awali kampuni hiyo ilikuwa inafuata huduma hiyo Afrika Kusini.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni katika ziara ya Waziri wa Madini, Doto Biteko ambaye alitembelea kampuni hiyo mkoani Geita kwa lengo la kujua maendeleo ya GGML baada ya  kuanza shughuli za uchimbaji wa chini ya ardhi katika migodi yake mitatu.

Akimkaribisha waziri huyo, Makamu Rais wa Anglo Gold Ashanti anayeshughulikia miradi endelevu kwa upande wa Tanzania na Ghana, Simon Shayo alisema mradi huo utaongeza mapato kwa serikali na kampuni hiyo kwa ujumla.

“Mradi huu wa kuchenjua mabaki ya kaboni unatusaidia kuhakikisha hatuyatupi mabaki ya dhahabu na mabaki yenye asili ya hewa ukaayanayoingia kwenye mazingira… kwa sababu dunianzima ipo kwenye mapambano ya kupunguza hewaukaa,” alisema.

Aidha, akizungumzia mradi huo, Dk. Biteko alisema awali kaboni zilizokuwa zinazalishwa  kwenye migodiiliyopo nchini zilikuwa zinasafirishwa kwenda nje yanchi.

“Tulizuia watu wakadhani tunafanya kitu kibaya, sasa GGML ameweka mtambo mpya ambao umegharimu Sh bilioni moja kwa ajili kuprocess  upya kaboni zadhahabu na kupata dhahabu safi badala ya kusafirishaile kaboni kupeleka nje ya nchi,” alisema.

Alisema mbali na manufaa ya mapato ambayo nchiinapata, pia watu wengi wameajiriwa kwenye mtambo huo na kuondokana na umaskini.

“Lakini pili teknolojia ya kaboni hizi ambazozinazalishwa kwenye migodi mingine zitakuwazinafanyiwa processing hapa nchini hasa ikizingatiwaile kaboni ina dhahabu.

“Mahali pengine unaweza kuona ile kaboni imetupwakama uchafu, lakini kwa taarifa tuliyopewa itazalishazaidi ya gramu 80,000, ni dhahabu nyingi zaidi ya kilo 80 kwa kaboni hii na bado itaendelea kuzalishwa mara nyingi. Kwa hiyo tutapata mapato mengi zaidi,” alisema na kuongeza;  

“Hakuna mgodi mwingine ambao umetengenezamtambo wa kuchenjua hiyo kaboni Afrika mashariki nakati kwa hiyo teknolojia hii sisi tumekuwa walimu, nawapongeza GGML kwa ubunifu huo,” alisema. 

Naye Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu (CCM) aliipongeza kampuni hiyo kwa hatua ilizochukua kuhakikisha kuwa inapanua wigo wa upatikanaji wa ajira kwa Watanzania.

“Mathalani tukizungumzia local content tulitaka iwe local of the local, nauona ushawishi huo unafanikiwa kwa sababu sasa katika maeneo mengi ambayo nimekwenda nimeona ushiriki wa watu wa Geita kwenye shughuli mbalimbali za uchumi wa mgodi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles