27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Mfuko wa NSSF wajipanga kumfikia kila mtu

Na Anna Ruasha, Geita

Serikali mkoani Geita imewakumbusha wachimbaji wadogo wa madini pomoja na wakazi wa Mkoa huo kutumia maonesho ya Tano ya Teknolojia ya Madini kutembelea banda la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili kupata elimu na kujiunga na mfuko huo kwa ajili ya kuweka akiba ya sasa na ya badae.

Wito huo umetolewa juzi na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Profesa Godius Kahyarara wakati akizungumza katika siku ya NSSF iliyowakutanisha wadau mbali mbali na wanachama wa mfuko huo wakati maonesho ya teknolojia ya madini yakiendelea mkoani humo .

“Ninyi wanachama tulioungana katika siku ya NSSF mkawe mabalozi wa kuhamasisha wananchi na wachimbaji wadogo kujiunga na mfuko huu, pia niwapongeze NSSF mmekuwa mkitumia maonesho haya kutoa elimu zaidi kwa wananchi kama mkoa huu,“amesema Kahyarara.

Kwa upande wake Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma wa NSSF, Lulu Mengele akizungumzia siku ya NSSF kupitia maonyesho hayo amesema lengo nikuendelea kuongeza uelewa kwa wanachama na wachimbaji wadogo wa madini kujiunga na mfuko huo.

Mengele amesema wametumia fursa ya maonyesho hayo kutoa elimu juu ya mfuko wa jamii na kuelezea umuhimu wa namna ya kujiunga na mfuko huo na kwamba kijana wa leo ni mzee wa kesho hivyo ni mujimu kuiiwekea akiba ya baadae huku akihimiza wanachama kuendelea kuchangia.

“Tumewafikia wananchi wa mkoa wa Geita ambapo wachimbaji asilimia kubwa sehemu ya wanachama wa NSSF na kuhusu huduma zetu ambazo zimekuwa zikitolewa kwa njia mbalimbali,” amesema Mengele.

Kwaupande wake Meneja wa NSSF mkoa wa Geita, Winniel Lusingu amesema wanaendelea kuhimiz wananchi kutambua umuhimu wa kujiunga na mfuko huo kwa kuwa unafaida kubwa katika maisha.

Ameongeza kuwa kupitia maonyesho ya Madini wanaendelea kuandikisha wanachama wapya kwa Sh 20,000 huku wakizingatia kauli mbiu ya ”Huduma bora ni kipaumbele chetu”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles