29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Filikunjombe: Sitaki urais 2015

Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe
Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe

NA MWANDISHI WETU, LUDEWA

MBUNGE wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), amesema katu hatamani kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Amesema bado anajiona anafaa zaidi katika nafasi ya ubunge na si urais kwani nafasi hiyo ya juu inahitaji ustahimilivu mkubwa, hasa kutokana na matumaini ya Watanzania kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hayo aliyasema juzi wilayani Ludewa, alipokuwa akizungumza katika misa ya kumuombea marehemu baba yake mzazi, Florian Filikunjombe, aliyefariki dunia Mei 5, mwaka huu.

Kauli ya mbunge huyo imekuja baada ya waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Manga ambao kutumia nyimbo kanisani hapo za kumtaka mbunge huyo awanie nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa nchi kutokana na kuwa ni kijana mwenye nguvu na uwezo katika taifa.

Alisema pamoja na kuombwa kuwania nafasi hiyo, lakini haitamani zaidi ya kuwatumikia wapiga kura wake wa Ludewa kwa kuhakikisha maendeleo yanapatikana chini ya uongozi wake.

“Ndugu zangu mnanitaka niwanie urais… Ni wazi ninapenda kutamka kwenu siko tayari na wala siitamani nafasi hii ya juu ila ninachoweza kusema kuwa mimi ninatamani ubunge kwani ndio nilioomba hapa Ludewa nanyi mnalitambua hilo.

“Ni kweli mimi ni kijana na nina nguvu, lakini suala la ujana haliwezi kuwa sifa za urais na uzee si sifa pia, ila mimi bado ndoto yangu ni kuona Ludewa yetu inabadilika na kupaa kwa maendeleo kama nilivyoahidi wakati mnanichagua miaka minne iliyopita.

“Urais si saizi yangu kwa sasa, si kama ninawagomea wenzangu ila ni bora niseme ukweli kwenu na hata kama Mungu atanichukua nafsi yangu itakuwa imesema ukweli mbele yake,” alisema Filikunjombe.

Mbali na kugomea nafasi hiyo, mbunge huyo alichangia Sh milioni 50 kwa ajili ya ukarabati wa Kanisa Katoliki Parokia ya Manga.

Filikunjombe alisema kazi ya ujenzi wa nyumba ya ibada ni muhimu na kila kiongozi anayetaka baraka ni lazima ashiriki kikamilifu.

Alisema bila kuchangia fedha hizo  kwa ajili ya ukarabati wa kanisa  hilo kuna hatari kwa waumini wa kanisa hilo kukosa sehemu ya kuendeshea ibada kutokana na jengo hilo baadhi ya sehemu kubomoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles