26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Ferguson: Klopp ameiweka Liverpool kwenye ubingwa EPL

alex-fergusonMANCHESTER, ENGLAND

ALIYEKUWA kocha wa timu ya Manchester United, Alex Ferguson, amesema kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, ameifanya timu hiyo kuwa wapinzani thabiti katika mbio za kuwania ubingwa Ligi Kuu England.

Kocha huyo alisema ameguswa sana na kazi anayofanya Klopp katika timu yake  na sasa amefungana pointi na Manchester City, baada ya kucheza michezo tisa ya ligi hiyo msimu huu.

Ferguson, anaamini timu tano za juu katika msimamo wa ligi hiyo zina nafasi ya kutwaa ubingwa, lakini ameipa nafasi kubwa Manchester City na Liverpool.

“Klopp amefanya kazi nzuri sana na ameamsha ari ya wachezaji wa Liverpool,” alisema Ferguson alipokuwa akihojiwa na jarida la Kicker kuhusu Klopp.

Ferguson aliongeza kuwa inawezekana klabu kubwa zikakosa ubingwa kwa miongo miwili.

“Sasa naweza kuwa na hisia njema kwamba mwaka huu Liverpool wamo kwenye hesabu za ubingwa. Unaweza kuona Klopp anavyojitoa, natumai kazi yake mazoezini ni njema pia kwani anao wasifu thabiti ambapo ni jambo muhimu sana kwa klabu kubwa kama hiyo,” alisema Ferguson.

Ferguson anatarajia ushindani mkubwa kwenye mbio za ubingwa, lakini hakuitaja Chelsea kama moja ya timu tishio kwenye ligi hiyo msimu huu.

“Miaka ya hivi karibuni ni vigumu kubashiri kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Nadhani kuna timu tano zenye nafasi kubwa, Manchester City nawapa nafasi kubwa, Tottenham na Liverpool lakini pia Manchester United bado wamo kama tukiwa na uthabiti,” alisema Ferguson.

Kocha huyo aliongeza kuwa msimu huu hata timu ikiwa nyuma kwa pointi sita au nane bado inawezekana kuzikamata timu zilizotangulia.

“Bila kuisahau Arsenal. Timu yao bado ipo imara na thabiti. Wako vizuri na ni timu inayotaka mafanikio. Navutiwa na kijana mdogo, Alex Iwobi,” alisema Ferguson.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles