NA FESTO POLEA, ZANZIBAR
MWANAMITINDO maarufu wa Zanzibar, Farouk Abdillahi, amesema wapo katika mpango wa kuanzisha mtaala wa mafunzo ya wabunifu wa mitindo ili kuendeleza na kukuza fani hiyo inayokabiliwa na changamoto nyingi katika utendaji kazi yake.
Farouk ambaye jana alizindua duka lake la nguo ikiwa ni mwendelezo wa matukio yanayofanyika katika tamasha la 19 la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF), alisema chuo hicho kitaanzia na elimu ya ngazi ya astashahada.
“Kwa sasa tunawafundisha baadhi ya wanafunzi wa mitindo lakini haitoshi ndiyo maana tumeona tuweke mtaala wa kufundisha masuala hayo katika Chuo cha Karume kilichopo hapa visiwani, lakini pia walimu wa taaluma hiyo watatoka nje,” alieleza mwanamitindo huyo.
Katika hatua nyingine jana mwanamitindo huyo alifungua duka lake la nguo na kitabu cha masuala ya mitindo cha mwanamitindo, Haji Gola, kilizinduliwa.