26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Bodi ya Filamu kumpa kazi Wakonta

Wakonta Kapunda
Wakonta Kapunda

MWANDISHI chipukizi wa miswada (script) anayeandika kwa kutumia ulimi, Wakonta Kapunda, amesema baada ya kumaliza mafunzo ya uandishi wa script, Bodi ya Filamu nchini imeahidi kumpa kazi ya kuandika script za filamu mbalimbali.

“Watendaji wa Bodi ya Filamu na Chama cha Wasanii wa Filamu (Taff), walikuja kunijulia hali akiwemo mkurugenzi wa bodi hiyo waliniahidi kwamba baada ya kumaliza mafunzo yangu watanipa kazi ya kuandika script za filamu mbalimbali nimefurahi kwa kweli kama watanipa kazi hizo,” alieleza.

Wakonta anasema kutokana na kuwa mwangaliaji wa filamu mzuri amegundua kwamba filamu zinabadilisha maisha ya wengi na zinaongeza faraja na kujenga kujiamini kwa maisha mapya ndiyo maana naye anataka kuwa mwandishi wa hadithi za kuleta faraja kwa kuwapa watu imani ya kuwa na maisha ya kutokata tamaa hata baya likiwakuta.

“Filamu ni maisha, inaweza kumjenga mtu kumliwaza na kumweka sawa kutoka kwenye majonzi, mimi nilikuwa mwangaliaji mkubwa wa filamu, nilikuwa nikiangalia zaidi waandishi wa script kutoka nje ya nchi na huko nilijifunza baadhi ya vitu lakini nilipokuja kwenye mafunzo ufahamu wangu wa uandishi ukaongezeka nashukuru kwa hilo na naona ndoto yangu inaelekea kutimia,” alieleza.

“Changamoto yangu kubwa kwa sasa ni vifaa vya kuandikia, natumia simu hii (anaonyesha) lakini pia ningepata baiskeli ya umeme ingenirahisishia zaidi kuliko hii ya kusukumwa wakati mwingine anayenisukuma huchoka,” alieleza Wakonta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles