Tunis,
SHIRIKA la Amnesty International linasema zaidi ya familia 100 zimeachwa ziangamie katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya.
Mawasiliano yamekatwa katika mji uligubikwa na vita wa Ganfouda kwa sababu ya vizuizi vilivyowekwa na vikosi vya waasi ambavyo ni tiifu kwa Khalifa Hefter.
Mgogoro umekuwa ukifukuta Benghazi kwa zaidi ya miaka miwili sasa kati ya majeshi yake na vikundi vya kiislamu vinavyoshikilia sehemu kubwa ya Mji wa Ganfouda.
Watu katika mji huo wameieleza Amnesty juu ya maisha mabaya wanayoishi huku kukiwa na ukosefu mkubwa wa mahitaji muhimu kama chakula na umeme.
Wengi wanatamani kuondoka sehemu hiyo lakini hawana uhakika wa usalama wao kwa sababu ya mapigano kushika kasi kubwa kati ya majeshi ya nchi hiyo na vikundi vya kiislamu.