27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Familia yambana Toure kuondoka England

koloLIVERPOOL, ENGLAND

BEKI wa klabu ya Liverpool, Kolo Toure, amedai kwamba anatamani kwenda kuicheza klabu ya Real Madrid, lakini familia yake ipo nchini England hivyo inamuwia vigumu kuhamia nchini Hispania.

Mkataba wa beki huyo unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu huu, lakini hadi sasa hajui msimu wa 2016-2017 atakwenda kuumalizia wapi.

Hata hivyo, klabu ya Liverpool kwa sasa ina wakati mgumu hasa katika safu ya ulinzi ambapo kuna baadhi ya wachezaji ni majeruhi kama vile Dejan Lovren, Martin Skrtel na Mamadou Sakho.

Mchezaji huyo anaamini kuwa kutokana na uwezo wake lazima atapata timu kubwa ya kuichezea baada ya kumaliza mkataba wake na Liverpool.

“Kama nitaendelea kucheza katika kiwango hiki cha sasa, lazima nitapata nafasi ya kujiunga na klabu ya Real Madrid, lakini sijui nini kitatokea mwishoni mwa msimu huu, ila napenda kuendelea kucheza Ligi Kuu England.

“Watoto wangu wapo hapa hivyo itakuwa ngumu kuondoka England na kujiunga na klabu nyingine, lakini kila kitu Mungu ndiye anayejua kwamba nitakuwa wapi baada ya kumaliza mkataba wangu, lakini ninaamini nitaendelea kucheza soka kwa kuwa napenda,” alisema Kolo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles