NA Elizabeth Joachim
Familia ya mwanamuziki wa muziki wa dansi, Ally Choki na uongozi wa bendi anayoifanyia kazi kwa sasa ya jijini Mwanza ya Super Kamanyola ya jijini Mwanza wamepanga kumrudisha mwanamuziki huyo Jijini Dar es Salaam katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uangalizi zaidi wa kimatibabu.
Mwanamuziki huyo alilazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kutokana akisumbuliwa na maradhi ya kisukali na Presha na ali yake ilipokuwa mbaya alikimbizwa chumba cha unagalizi maalum (ICU) lakini sasa anaendelea vyema.
“Ndugu yetu anaendelea vyema lakini kwa sasa tupo katika kikao maalum kati ya mimi kaka wa familia na uongozi wa bendi anayoifanyia kazi kwa sasa na lengo ni kumrudisha kwanza hospitali ya Muhimbili ili pate uangalizi zaidi wa kimatibabu kisha akitengamaa kiafya atarudi kuendelea na kazi yake katika bendi mpya,’’ alisema Hamad.
Kaka wa mwanamuziki huyo, amesema hali ya mdogo wake ilikuwa mbaya na ilihitaji usaidizi wa karibu mno ndiyo maana wanalazimika kumpeleka hospitali ya karibu na ndugu zake kwa ajili ya uangalizi na faraja ili arudishe afya yake kwa haraka.
Ali Choki alianza kujisikia vibaya Ijumaa iliyopita na kabla ya kukimbizwa katika hospitali hiyo alifikishwa hospitali binafsi jijini humo.
Amesema alipofikishwa Bugando ndugu yake huyo alikosa hewa hivyo akawekewa hewa ya Oxgen na kisha akawekwa chumba cha wagonjwa mahutiti (ICU).