27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, September 22, 2024

Contact us: [email protected]

Fadlu awatoa hofu wanasimba kuhusu ubingwa

Na Mwandishi Wetu

Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema mchezo wa kesho dhidi ya APR  katika  kilele cha  tamasha la Simba Day, utatoa picha  kuelekea msimu 2024/25, huku  malengo yakiwa ni kutwaa ubingwa.

“Ninafahamu Simba haijatwaa taji la ligi kwa miaka mitatu lakini safari hii tuna timu bora ambayo najivunia kuwa itatupeleka kwenye malengo tuliyojiwekea,” amesema.

Katika mchezo huo Fadlu amesema  atatoa nafasi kwa  wachezaji wote ili kuzoea mazingira ya kucheza mbele ya mashabiki wengi.

“Kikosi kipo kwenye hali nzuri, mchezo wa kesho utakuwa kipimo bora kwetu, tunafahamu mashabiki watajitokeza kwa wingi uwanjani nasi tunaona itakuwa jambo zuri kuwapa furaha ya ushindi.”

Kwa upande wake nahodha wa timu, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amewatoa hofu Wanasimba na  akijivunia kikosi cha kuwa ni imara ya ushindani na kesho wataanza kupata furaha waliyokuwa wanaisubiri.

“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua kuwa ni sikukuu ya Wanasimba na tiketi zimeisha siku tatu kabla kwa hiyo wachezaji tunajua tuna jambo kubwa la kufanya,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles