Na JOSEPH LINO
KWA wanafunzi ambao wanatamani kusoma nje lakini hawana uwezo wa kutosha kujilipia ada, ufadhili wa masomo (scholarships) unakuwa msaada w akutosha kutimiza ndoto zao.
Kuna scholarships ambazo zinapatikana kwa wanafunzi wachache na hii inafanya kuwa na ushindani mkubwa ili kupata.
Kuna mambo mengi unahitaji kufanya na kuzingatia ili uwe na nafasi kubwa ya kupata ufadhili.
Haya ni baadhi ya makosa hufanywa na wanafunzi wakati wa kuomba scholarship.
Kutofanya utafiti
Wanafunzi wengi hawana ufahamu wa kujua nafasi ya scholarships zinapatikana sehemu husika anayotuma maombi.
Ndio maana unahitaji kufanya utafiti wa kutosha kwenye mitandao ikiwamo ya kijamii au tovuti.
Kampuni na taasisi hutoa ufadhili kwa wanafunzi wasiojiweza hivyo, wanakuwa makini kufuatilia.
Hii inafanywa pia na vyuo vikuu, pamoja na mashirika ya kitaaluma. Pia ni vizuri kutafuta washauri wa elimu ili kupata taarifa zaidi ya ufadhili wa masomo.
Mwishoni unaweza kuwa na fursa kadhaa za kupata ufadhili wa masomo kwa nafasi kubwa.
Kuangukia kwenye fadhili wa uongo
Kila mwaka, maelfu ya watu huathirika na wadanganyifu wa mitandao kwa kutoa ufadhili wa masomo ambao si wa kweli.
Jihadhari na ishara kama vile kukuhakikishia kuwa utapata, pia kuomba kadi ya ATM au taarifa za benki yako, kulipa ada ya maombi au kupata ofa bila kuomba ufadhili wa masomo fulani.
Kuangalia matokeo yako
Wafadhili wengi huwa na vigezo maalumu kwa waombaji, kuanzia kozi utakayosoma hadi nchi unayotaka kwenda kusoma.
Ni jambo la muhimu kuhakikisha unakidhi vigezo vya ufadhili ili usipoteza muda wako na juhudi. Hivyo, hakiki kwa kuangalia kwamba unasifa za kutosha kutuma maombi.
Lazima pia kuangalia mahitaji mengine, kama vile utahitaji kuambatanisha nyaraka zingine kabla ya kuwasilisha maombi yako.
Kujaziwa fomu
Wakati wa maombi ya ufadhili wa masomo, tunaelewa kama unajaribu kwa kupata msaada kutoka kwa watu wa karibu kujaza fomu, kwa mfano wazazi kunaweza kuleta shida.
Hata hivyo, haishauriwi kufanya hivyo kwa sababu wewe unakwenda chuo kikuu hivyo utapaswa kuwa na uwezo wa kujaza fomu yako mwenyewe.
Unaweza kufanya hivyo lakini mbali na hilo, baadhi ya wafadhili wanaweza kukuita kwa ajili ya usaili ukiwa ni miongoni mwa waliochaguliwa.
Kutumia insha iliyotumika ni vizuri, lakini si kwa ajili ya maombi ya ufadhili wa masomo.
Waamuzi wanatambua vizuri. Soma vizuri kuhusu shirika hilo ambalo linatoa ufadhili na kitu gani wanataka katika insha hiyo, ili uweze kuandika insha yako kulingana na mahitaji yao.
Hakikisha unaandika insha yako katika njia ambayo itawashawishi wao kwamba wewe unastahili zaidi.
Kuwa na uhakika na malengo na ndoto zako, kuwa wazi na mifano mifupi na wala usihangaike kutumia maneno magumu.
Kagua maombi yako kabla ya kuwasilisha Moja ya kosa kubwa ni kupeleka maombi ambayo yamejaa makosa ya kisarufi. Kwa majaji, utaonekana kwamba hukuwa na juhudi au haujali kama utapata au hupati.
Angalia maelezo yako yote na hakikisha yapo sahihi, kama vile anwani na namba za mawasiliano.
Pia, linapokuja suala la barua pepe, wala usitumia maneno yenye taswira tofauti kama [email protected] hii inaweza kusababisha maswali mengi.
Akaunti yako ya mtandao wa kijamii kuchunguzwa Kama wewe unatafuta ufadhili, wanaweza kuchunguza taarifa na akaunti zako kwenye mitandao maarufu ya kijamii.