29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

EMMANUEL OKWI AMEWAHI KUWAPOTEZA MAKIPA HAWA

NA MARTIN MAZUGWA-DAR ES SALAAM


SI ajabu kumuona mchezaji fulani aking’ara katika mechi tofauti, lakini baada ya muda mfupi akipotea na hata kusahaulika katika vinywa vya wapenzi wa mchezo wa soka.

Zipo sababu nyingi zinazowafanya wachezaji kupotea kwenye ramani, lakini kwa upande wa walinda mlango kinachowapoteza ni kitendo cha kufungwa mabao ya utata.

Hali hii ndio inayowakuta makipa wengi wa bongo, moja kati ya washambuliaji wanaoongoza kwa kuwapoteza makipa hapa nchini ni Mganda, Emannuel Okwi nyota anayecheza katika kikosi cha Simba hivi sasa, akitokea klabu ya SC Villa.

Okwi ambaye amerejea katika kikosi cha Simba kwa mara ya tatu ndani ya misimu tisa akicheza katika timu za Etoile du Sahel, Sonderjyske, Yanga pamoja na SC Villa iliyomkuza tangu alipokuwa kinda.

Wafuatao ni walinda mlango waliokutana na dhahama ya kupoteza namba katika kikosi cha kwanza, baada ya kufungwa mabao ya kizembe na Okwi.

Ali Mustapha ‘Barthez’ (Yanga SC)

Ni kati ya makipa bora kuwahi kutokea katika nchi ya Tanzania, kutokana na ubora wake anapokuwa langoni kwa kutoa michomo hatari, lakini pia mwenye uwezo mkubwa kudaka penati.

Barthez ambaye ni kipa wa zamani wa ‘wauza mitumba’ wa jiji la Dar es Salaam, Ashanti United, Simba SC pamoja na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga alikuwa na wakati mzuri zaidi alipokuwa Yanga, akiaminiwa kutokana na uzoefu wake kabla ya Okwi hajamtibulia.

Kipa huyo aliweza kupotea, mara baada ya mshambuliaji raia wa Uganda, Okwi,  alipomfunga bao pekee lililoiwezesha Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, msimu wa 2014-15.

Mara baada ya bao hilo, mlinda mlango huyo alipoteza namba katika kikosi cha kwanza na kumuacha Deogratius Munishi ‘Dida’ akivaa viatu vyake, huku pia akishindwa kuendelea kuwepo kwenye kikosi cha Yanga hadi pale alipoamua kuondoka na kwenda kujiunga na  Singida United iliyopanda daraja msimu huu.

Mwadini Ali Mwadini (Azam fc)

Kwa miaka miwili ya mwanzo aliyojiunga na Azam FC, Mwadini alionekana ndiye kipa bora katika soka la bongo, lakini alijikuta hana nafasi tena ndani ya timu yake hiyo hadi sasa, baada ya kufungwa  bao la kizembe na Okwi katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2012/13.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Simba iliweza kupata ushindi wa mabao 2-0 ambayo yote yalipachikwa na mshambuliaji huyo raia wa Uganda, ambaye pia msimu huu ameanza na kasi ya aina yake ya upachikaji mabao akiwa na mabao sita, huku akiongoza orodha ya wafungaji.

Mara baada ya bao hilo Mwadini alipoteza namba mbele ya kipa namba mbili, Aishi Manula,  ambaye hadi anaondoka Chamazi Complex na kujiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili msimu huu wa ligi, alionekana ndiye namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC.

Lakini mbali na kupoteza namba katika kikosi hicho cha ‘Waoka mikate’, pia amepoteza namba katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Said Mohamed (Mtibwa Sugar)

Mlinda mlango huyo wa zamani wa timu za Majimaji , Yanga pamoja na Mtibwa Sugar ni mmoja wa makipa waliopotezwa na Okwi, ambaye hivi sasa wanakipiga katika klabu moja ya Simba akitokea Mtibwa Sugar.

Alikuwa mlinda mlango wa kuaminika katika kikosi cha Mtibwa Sugar chini ya kocha Mecky Mexime, alifungwa bao la Kizembe katika ushindi wa bao 1-0 msimu wa 2012-13 na kupoteza namba mbele ya Hussein Sharif ‘Casillas’.

 

 

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles