25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Elimu ya matumizi sahihi ya Mazingira yahitajika kulinda viumbe hai

Na Editha Karlo, Mtanzania Digital

Matumizi mabaya ya mazingira yanayofanywa na binadamu yanachangia wanyama na viumbe hai mbalimbali kupotea na hata baadhi yao kufariki.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), Dk. Ellen Otaru, ambaye amesema kuwa kwenye mkutano uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam uliowashirikisha waandishi wa habari 25 kutoka vyombo mbalimbali nchini.

Mkutano huo ulikuwa ukihusu uhifadhi, uwindaji haramu wanyamapori na usafirishaji kwa kupitia mradi wa USAID tuhifadhi Maliasili ambao unatekelezwa na JET kwa muda wa miaka mitano.

Amesema asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana na ndio mtegemeo la Taifa, mambo ya kijamii yanaongezeka kila siku lakini ardhi bado inaendelea kubaki hivyo hivyo hali inayopelekea kugusa maeneo ya uhifadhi maliasili, hivyo kuna haja ya kuangaliwa upya mipango miji na kuwepo kwa maeneo maalumu ya uhifadhi.

Amewataka wanahabari baada ya mafunzo hayo kutumia kalamu zao kwa kuandika habari zitazoigusa jamii kuendeleza kuifadhi maliasili kwaajili ya vizazi vijavyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo amesema kuwa waandishi wanayo nafasi kwa kutumia kalamu zao kwa kuandika habari habari za kuelimisha umma kuachana na matukio ya uwindaji haramu.

Chikomo alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari wa kusimamia na kuandika habari za uhifadhi,uwindaji haramu na usafirishaji wa wanyama pori ili jamii iweze kufahamu changamoto kubwa inayoikumbuka sekta ya uhifadhi wa maliasili.

Mtaalamu kutoka mradi wa USAID Tuhifadhi maliasili Joseph Olila aliwataka waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele kupaza sauti kwa jamii kwa kuandika habari zenye kuifanya jamii itambue mipaka yao na wanyamapori.

“Wanahabari nyinyi mnayo fursa ya kupaza sauti kwa umma katika hili suala la ushiriki wa kusimamia mchakato wa kupanga ardhi kwa manufaa ya wanyama,ili watu waelewe shughuli za kibinaadam hazipaswi kuzidi mipaka”alisema Olila

Naye Ofisa Mtandao wa Ufuatiliaji biashara ya wanyamapori, Allen Mgaza wakati akiwasilisha mada yake amesema kuwa waandishi wanatakiwa kuibua biashara haramu za viumbe bahari na wanyama ambavyo vimepigwa marufuku lakini kuna baadhi ya wananchi wanaifanya kwa kujua au kwa kutokujua.

“Kuna viumbe bahari baadhi ni maarufu kuvifanyia biashara lakini vinauzwa mtaani,pia kuna watu wanauza mafuta ya simba kama dawa,kucha za simba,ngozi za chui na siyo rahisi kuwagundua,ila ninyi waandishi hiyo ni kama “tip” mnaweza ifuatilia na kuandika habari za kuelimisha jamii,” amesema Mgaza.

Nao waandishi wa habari za uhifadhi, uwindaji haramu wa wanyamapori na usafirishaji wameushukuru mradi wa USAID tuhifadhi Maliasili pamoja na chama cha waandishi wa habari za mazingira Tanzania (JET) kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yameweza kuwajengea uelewa juu ya uhifadhi wa wanyama pori.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles