21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Ebola bado ni changamoto DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ana wasiwasi mkubwa juu ya idadi mpya ya wagonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake mjini New York, Marekani hii leo, Katibu Mkuu amesisitiza kuwa Umoja wa Mataifa unaendelea na jitihada zake za kudhibiti Ebola huko Kivu Kaskazini nchini DRC.

Ripoti zinasema kuwa mwezi 10 sasa tangu mlipuko wa ugonjwa huo zaidi ya watu 1000 wamefariki duniani ambapo Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa.

Hata hivyo Guterres amepongeza serikali ya DRC, taasisi zake na wananchi kwa hatua za kudhibiti ugonjwa huo ambao ulikumba pia jimbo la Ituri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles