25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Dulla Mbabe kuzichapa fainali Championi wa Kitaa kesho

NA WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi maarufu Dulla Mbabe anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa dhidi ya Amour Haji katika pambano la kusindikiza fainali ya Champion wa Kitaa itakayofanyika kesho Machi 20,2022 kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Zaidi ya mabondia 30 watakaopanda ulingoni siku hiyo, wamepima uzito leo Machi 19,2022 kwenye viwanja vya Las Vegas Mabibo, huku kila mmoja akitamba kumtwanga mpinzani wake na kutawazwa kuwa Championi wa Kitaa.

Kati ya mapambano hayo, matano ndiyo yatakuwa ya kusaka Championi wa Kitaa, huku mengine yakiwa ni wasindikizaji.

Pambano kubwa katika usiku huo litakuwa kati ya Salehe Mkalekwa dhidi ya Maono Ally, huku James Kibazange na Ally Ngwando wakipata ofa ya kupigania mkanda wa PST baada ya kuonekana kupata sapoti kubwa ya mashabiki.

James Kibazange(kushoto) akitunishiana misuri na Ally Ngwando baada ya kupima uzito leo

Kibazange na Ngwando ambao ni mabondia vijana ambao wameonekana kufunika kwa kuwavutia mashabiki wengi wa masumbwi waliojitokeza wakati wa kupima uzito kutokana na upinzani walionao, kila mmoja akiapa kummaliza mwenzake mapema.

Akizungumzia maandalizi yake, Kibazange amesema amefanya mazoezi kwa muda mrefu na malengo yake ni kumaliza pambano hilo la raundi nane kwa K.O.

“Ninachowaambia mashabiki wangu kuwa mimi sijawahi kuwaangusha, nawaahidi huyu mtoto sidhani kama atamaliza raundi nane, nampiga K.O mapema naondoka,” ametamba Kibazange.

Naye Ngwando amewataka mashabiki wake wajitokeze kwa wingi kwa sababu mtu aliyekuwa anamkimbia kimbia siku nyingi ameingia katika anga zake.

Pambano lingine la kisasi ni kati ya Dulla Mbabe kutokana na mpinzani wake Amour kutamba kuwa anataka kulipiza baada ya mara ya mwisho kuchezea kichapo kutoka kwa mbabe huyo.

Salehe Mkalekwa (kushoto) akitunishiana misuri na Maono Ally baada ya kupima uzito leo

Aidha muandaaji wa mapambano hayo, Meja Selemani Semunyu, amesema kutokana na sapoti na ushirikiano wa mashabiki ameamua kutoa zawadi ya kugombania mkanda kwa Kibazange na Ngwando.

Amesema kesho atatangaza zawadi nyingine endapo mashabiki wa ngumi watajitokeza kwa wingi kumuunga mkono na kuwasapoti vijana.

Pia amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kwani ndiyo itakuwa siku ya utambulisho rasmi wa pambano la Twaha Kuduku na Alex Kambangu litakalopigwa Machi 26, 2022, Morogoro.

Ametaja kiingilio cha chini katika pambano hilo ni sh 5000, huku cha juu kikiwa sh 10,000 kwa mtu mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles