28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

DROGBA ATHIBITISHA KUONDOKA MONTREAL IMPACT

MONTREAL, CANADA


 

didier-drogbaNYOTA wa zamani wa klabu ya Chelsea, Didier Drogba ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Montreal Impact, amethibitisha kuwa hana mpango wa kuendelea na klabu hiyo katika msimu wa 2017.

Mchezaji huyo juzi alishuka dimbani na kucheza mchezo wake wa mwisho kabla ya kuchukua kipaza sauti na kuwaaga mashabiki na wadau ambao walijitokeza kwenye mchezo huo kati ya Montreal Impact dhidi ya Toronto FC.

Katika mchezo huo ulihudhuriwa na jumla ya watazamaji 61,104 katika Uwanja wa Olympic, ambapo klabu ya Montreal Impact ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Inadaiwa kwamba mashabiki wengi ambao walijitokeza uwanjani hapo walikuwa hawajui kama mchezaji huyo anataka kuwaaga, hivyo walishangaa kuona anawaaga, hata hivyo mchezaji huyo alisema kuwa kwa sasa ataendelea kuwa katika klabu hiyo hadi pale mkataba wake utakapomalizika Desemba mwaka huu.

“Mkataba wangu unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo siwezi kuendelea tena na klabu hii,” alisema Drogba baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na mashabiki wake baada ya mchezo huo kumalizika.

“Nataka kumaliza vitu vyangu vizuri, kama vile kuacha heshima na watu wangu wa klabu hii, watu wa hapa mjini ambao walionesha ushirikiano mkubwa kwangu, nilikuwa najisikia vibaya na matokeo, lakini nashukuru tumefanikiwa kufuzu kwenda fainali,” aliongeza.

Nahodha wa klabu hiyo ya Impact, Patrice Bernier, ambaye alikuwa ni mchezaji wa kwanza kujua kwamba mchezaji huyo hana mpango wa kutaka kuendelea na klabu hiyo msimu ujao, alimmwagia sifa nyota huyo mwenye umri wa miaka 38 kwa mchango wake na kuweza kuwaweka wachezaji katika umoja tangu alipojiunga na timu hiyo.

“Didier amefanya makubwa sana uwanjani na nje ya uwanja, anafaa kuwa kiongozi kutokana na uzoefu wake na ameweza kutengeneza ubinadamu ndani ya timu, ni jambo la kujivunia kuwa na mchezaji kama huyo ndani ya timu, tunatamani kumuona akiendelea kucheza ndani ya klabu hii hata kwa michezo miwili au mitatu,” alisema Bernier.

Drogba aliongeza kwa kusema, ana furaha kubwa kuona timu hiyo akiiacha ikiwa katika mazingira mazuri na anaamini wachezaji waliopo wataendelea kufanya hivyo na kuipeleka mbali zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles