HASSAN DAUDI NA MITANDAO
BAADA ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May, kuweka wazi kuwa ataachia ngazi, kuna orodha ndefu ya wanaohusishwa na wadhifa huo.
Mwanamama huyo alifichua mpango wake huo siku chache zilizopita, akisema ataachana na jukumu la kukiongoza Chama cha Conservative, ifikapo Juni 7, mwaka huu.
Inaeleweka kuwa uamuzi wake huo ulikuja baada ya kufeli kwa jaribio lake la mwisho la kusaka ushawishi wa mpango wa kuiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya (EU), maarufu kwa jina la Brexit.
Hata hivyo, May atabaki kuwa Waziri Mkuu hadi pale atakapopatikana kiongozi mpya wa Chama cha Conservative, mchakato ambao unaweza kuchukua muda kidogo.
Ikumbukwe kuwa atakayeukwaa wadhifa huo atatokana na uchaguzi utakaofanyika bungeni, hivyo wingi wa kura za ndiyo ndiyo mshindi atapatikana kwa idadi ya wawakilishi watakaomuunga mkono ‘mjengoni’.
Tukirejea katika orodha ya wanaopewa nafasi kubwa ya kukilia kiti chake, wachambuzi wa siasa za kimataifa wanamtaja aliyekuwa Katibu wa Brexit, Dominic Raab.
Baadhi ya wachambuzi wanamtaja Raab licha ya kutambua wazi kuwa anakabiliwa na upinzani mkali anaoutazamiwa kuupata kutoka kwa Boris Johnson, Paddy Power, Michael Gove, Jeremy Hunt, Sajid Javid, Andrea Leadsom na Penny Mordaunt.
Ni kwa maana hiyo basi, Raab naye anahesabika kuwa anaweza kwenda kukiongoza Chama cha Conservative, kiti anachokiacha mwanamama May.
Hata msomi huyo wa sheria mwenye umri wa miaka 45 ameweka wazi nia yake hiyo ya kuiongoza Uingereza endapo May ataondoka.
“Nitalitanguliza jina langu kuwa waziri mkuu. Uingereza ni kama imekwama, hivyo inatakiwa kupata uelekeo mpya,” alisema Raab katika moja ya mahojiano yake na kituo cha televisheni.
Raab anafahamika machoni mwa wafuatiliaji wa siasa kuwa ni miongoni mwa waumini mkubwa wa mpango wa taifa hilo kujitoa EU.
Akisisitiza umuhimu wa kujiondoa kwao katika Umoja huo, mwanasiasa huyo alisema: “Tutakuwa vizuri zaidi tukiwa huru kufanya biashara, ikizingatiwa kuwa kumekuwa na ukuaji mkubwa wa masoko ya Latin Amerika na Asia.
Si tu alisema hatua hiyo itaiwezesha Uingereza katika kutengeneza ajira kwa watu wake, pia aliongeza kuwa vimekuwapo vitendo vya rushwa ndani ya EU.
Huku akisema mtangulizi wake, May, hakuwa imara kuukamilisha mpango wa kujitoa EU, Raab ameahidi kuwa hataomba kuongezewa siku za kujitenga na Umoja huo.
Ukiacha May, pia mwanasiasa huyo aliinyooshea kidole timu nzima iliyokuwa ikiusimamia mpango huo, akiitaja kuwa ilikuwa ikimpuuza.
Aidha, katika mwendelezo wa ahadi zake za kuisaka nafasi ya May, amesema endapo atachaguliwa, basi atahakikisha anawapunguzia wafanyakazi wa Uingereza mzigo mkubwa wa kodi.
“Tunapaswa kupunguza kodi ili kuwapa wafanyakazi wa kipato cha chini au cha kati fursa ya kukuza uchumi wao, jambo ambalo wengi wameshindwa kulifanya kwa miaka sasa,” alisema.
Wakati huo huo, alisema anaamini anaweza kukiunganisha Chama cha Conservative na Chama cha Unionist na atakuwa tayari kuupeleka mbele mpango wa Brexit na kuiongoza Uingereza aliyoitaja kuwa ni taifa kubwa katika uso wa dunia.
Wengi wanaukumbuka uchapaji kazi wake akiwa Wizara ya Mambo ya Nje, ambapo alishiriki kwa kushahuri migogoro mbalimbali, ukiwamo ule wa Waarabu na Israel.
Aidha, katika kuyaweka mbele masilahi ya Uingereza, jambo linalompa mvuto mbele ya wananchi, itakumbukwa kilichotokea mwishoni mwa mwaka jana.
Raab alisema ni kweli mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi, yanasikitisha, lakini nchi yake haiwezi kuwatupia lawama washukiwa (Saudi) na kuharibu ukaribu wao.
“Serikali ya Uingereza haitatupia mkono na kuharibu uhusiano uliopo na Saudi Arabia,” alisisitiza Raab, ambaye ni pia ni mchezaji wa mchezo wa karate akiwa na mkanda mweusi.
Baba mzazi wa Raab ana asili ya Jamhuri ya Czechoslovakia na Israel na aliingia Uingereza akiwa mkimbizi, kipindi ambacho alikuwa na umri wa miaka sita.
Hapa ni Raab akisimulia mkasa wa mzee wake, Peter, kuhamia Uingereza. “Mwaka 1938, Kikundi cha Nazi cha Ujerumani kiliivamia Czechoslovakia. Bahati ni kwamba wananchi wengi walikimbia Uingereza.
“Familia moja ya Kiyahudi ilifika Uingereza ikiwa na kija mdogo aitwaye Peter. Alikuwa na umri wa miaka sita tu na hakuwa akizungumza Kiingereza.
“Kijana mdogo huyo ndiye baba yangu. Nitaiheshimu kumbukumbu yake kwa kupambana dhidi ya ubaguzi wa rangi hadi pumzi yangu ya mwisho.”
Kutokana na historia yake hiyo, amesema atakapoingia madarakani atapambana kwa kadiri atakavyoweza kuhakikisha jamii yenye usawa, hasa kwa kuzipa nguvu familia masikini na vijana wasio na ajira.
“Baba yangu alikuja hapa akiwa mkimbizi akiwa na umri wa miaka sita akiwa hajui Kiingereza. Lakini, Uingereza ilimpa hifadhi na fursa kupitia shule na kazi.
“Hakuna mzazi wangu aliyefika chuo kikuu lakini wote walifurahia maisha, walinunua nyumba, walikuza familia na waliishi katika ndoto za Uingereza. Vijana wengi hawapati hiyo kwa sasa,” alisema.
Lakini sasa, hiyo haitoshi kumfanya Raab kuwa mwanasiasa asiye na wakosoaji. Mwanzoni mwa mwaka 2011, gazeti la Mail lilichapisha andiko stori iliyomtaja aliwahi kumpa mwanamke kiasi cha Pauni 20,000 ili tu asifichue vitendo vya kiudhalilishaji alivyomfanyia.
Gazeti hilo liliibua kuwa mbali ya kupewa fedha, pia ulikuwapo mkataba uliomtaka mwanamke huyo aliyekuwa mfanyakazi wake kutoizungumzia kokote siri hiyo.
Baba huyo wa watoto wawili alikanusha vikali tuhuma hizo akisema zililenga kumchafua, ikifikia hatua ya kukishitaki chombo cha habari hicho, kabla ya kufanikiwa kukifungia baada ya rufaa yake kutupiliwa mbali na Mahakama Kuu.
wadhifa huo atatokana na uchaguzi utakaofanyika bungeni, hivyo wingi wa kura za ndiyo ndiyo mshindi atapatikana kwa idadi ya wawakilishi watakaomuunga mkono ‘mjengoni’.