29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Dola milioni 75 kuleta mapinduzi elimu ya ufundi Afrika Mashariki

Asha Bani-Dar es salaam

Serikali ya Tanzania imepewa kiasi Dola za kimarekani milioni 75 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kuleta mapinduzi katika elimu ya ufundi Afrika Mashariki (Eastrip).

Akizungumzia mradi huo leo  kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Katibu Mkuu wa wizara hiyo  Dk .Leornad Akwilapo amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kuvijengea vyuo vya ufundi uwezo, kuongeza idadi ya wanafunzi ,kujenga miundombinu bora katika vyuo hivyo sambamba na kupata wahitimu wenye uzoefu  watakaoweza kujiajiri na kuajiriwa bila wasiwasi.

Dk. Akwilapo alisema fedha hizo zitapelekwa katika vyuo vinne nchini ikiwa ni pamoja na Chuo cha Ufundi nchini(DIT) kampasi ya dar es salaam na Mwanza, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Dar es salaam, Chuo cha Ufundi Arusha (ATC).

“Tunawashukuru benki ya dunia kwa maana fedha hizo zitatumika katika kuhakikisha wanawajengea uwezo wanafunzi na pindi wanapohitimu inakua rahisi kuajiriwa viwandani na hasa ikizingatiwa tanzania inaelekea  katika uchumi wa viwanda kwa sasa,”

“Watanzania wanatakiwa kufahamu kwamba vyuo vya ufundi visiwe chaguo  la mwisho kwa mtu anayefeli bali viwe vyuo ambavyo vinaweza kumsaidia kijana  kujiajiri mwenyewe na hata kuajiriwa na jambo ambalo ni zuri kwa nchi yetu ,”amesema Dk. akwilapo.

Naye mratibu wa mradi Dk. Noel  Mbonde amesema vyuo hivyo vinne vimejikita katika masuala ya teknolojia ya habari(Tehama), gesi asilia, ngozi  na masuala ya anga.

Naye mhadhiri wa chuo cha DIT Dar es salaam, Dk. Joseph Matiko amesema fedha hizo walizokabidhiwa wao ni kwa ajili ya kujenga miundombinu itakayoendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia chuoni hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles