22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji yavutiwa na Stamigold

MWANDISHI WETU-BIHARAMULO

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC), imeridhishwa na maendeleo ya mgodi wa Stamigold, baada ya uongozi wake mpya kuweza kupunguza kwa kiasi kikubwa gharama za uendeshaji.

PIC ilikutana na uongozi wa mgodi huo Oktoba 30 jijini Dodoma na Novemba 17 mwaka huu, kamati hiyo ikatembelea mgodi huokujionea hatua ambazo zimefi kiwa.

Katika ziara hiyo, kamati iliambatana na Waziri wa Madini, Doto Biteko, Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugenzi wa Sera na MipangoWizara ya Madini, Augustine Ollal, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Meja Jenerali (Mstaafu) Michael Isamuhyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO,

Dk. Venance Mwasse na Mkuuwa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde.

Akitoa taarifa kwa kamati hiyo, Mkuu wa Mgodi wa Stamigold, Mhandisi Gilay Shamika, alisema menejimenti ya mgodi huo imefanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua uwepo wa dhahabu katika sampuli vya mgodi huo.

Alisema kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa kwenye maabara ya The African Minerals and Geo-sciences Centre (AMGC) zamani SEAMIC mwaka 2018, imebainisha uwepo wa wastani wa wakia 200,000 za dhahabu kutoka

kwenye bwawa la visusu (Tailings Storage Facility) lenye ujazo wa tani

8,600,000.

Shamika alisema kwa sasa, mgodi umeshandaa Mpango wa Biashara mahususi kwa ajili ya kuchenjua visusu hivyo.

“Mpango huo unaelezea makadirio ya mapato yatakayopatikana, gharama na faida zitakazotokana na mradi huo.

“Visusu hivyo vinakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Marekani milioni 260 na vinaweza kuchenjuliwa kwa miaka saba kulingana na tafi ti mbili tofauti

zilizofanyika kwa wakati tofauti ili kujiridhisha na makisio hayo,”

alisema Shamika.

Shamika alisema katika mwaka wa fedha wa 2018/19 jumla ya wakia 13,194.58 za madini ya dhahabu na wakia 1,813.57 za madini ya fedha

zenye thamani ya Sh bilioni 38.3 zimezalishwa na kuuzwa na mgodi huo.

Alisema mpango wa mgodi ni kuzalisha wastani wa wakia 1,200 kwa mwezi (sawa na wakia 14,400 kwa mwaka) ili kukidhi gharama za uendeshaji na kupata faida katika mwezi husika.

“Kwa mwaka wa Fedha 2018/19 mgodi ulivuka malengo kwa kuzalisha wakia 15,008.15 ambapo wakia 13,194.58 zilikuwa za madini ya dhahabu na wakia 1,813.57 za madini ya fedha zote zenye thamani ya Sh bilioni 38.4,” alisema Shamika.

Alisema uongozi wa STAMIGOLD umeendelea kupunguza gharama za uzalishaji na uendeshaji wa mgodi ambapo zimepungua kutoka wastani wa

dola za Marekani (1,800 kwa wakia moja katika kipindi cha Januari hadi Machi, 2018 na kufi kia wastani wa USD 940.14 kwa wakia moja katika kipindi cha Julai 2018 hadi Juni, 2019.

Alisema mgodi unaingia gharama kubwa za uendeshaji kutokana na matumizi ya nishati ya mafuta.

“Mgodi unatumia wastani wa lita 15,000 za mafuta kwa siku ili kukamilisha shughuli za utendaji za kila siku. Matumizi hayo ya mafuta

yanaugharimu mgodi takriban Sh bilioni 1 kwa mwezi,” alisema Shamika.

ma mpango wa kuunganishiwa umeme utakapokamilika, gharama za umeme zinatarajiwa kupunguza kwa Sh milioni 700 kwa mwezi.

KAMATI YAWAVULIA KOFIA

Katika maazimio ya kamati na mgodi yaliyofanywa Novemba 18 mjini Geita, kamati hiyo pamoja na kuonyesha kuridhishwa kwake na hatua zilizopigwa na mgodi, pia ilitoa maagizo kwa uongozi wa mgodi huo ambao unamilikiwa na Serikali na kuendeshwa na Watanzania kwa asilimia 100.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Dk. Raphael Chegeni na Makamu Mwenyekiti, Zainabu Vullu, pamoja na mambo mengine waliwataka wafanyakazi kujituma zaidi ili kuhakikisha wanafi kia malengo waliyojiweka.

“Kamati pia itatoa ushirikiano kila inapohitajika,”alisema Dk. Chegeni.

Pia kamati hiyo ilitaka uchimbaji na utafi ti kwenye mgodi huo ufanyike kwa pamoja na ilipongeza hatua ya kupunguza gharama za uendeshaji wa mgodi huo ambao kabla ya uongozi mpya zilikuwa juu hadi Serikali ikafi kiria kuufunga.

Kamati pia ilitaka utekelezaji wa mradi wa visusu, ili fedha za dola za Marekani milioni 260 zipatikane kama ambavyo inakadiriwa na wataalamu wa mgodi huo kuwa mradi huo utaingiza fedha hizo.

Ilitaka pia baada ya utafi ti kukamilika kuwe na eneo jingine zaidi la kuchimba madini hayo ya dhahabu tofauti na lile ambalo sasa linachimbwa.

“Kuhusu kuuza madini kwenye soko la ndani, mjitahidi hilo liwe limeanza kutekelezwa kabla ya mwisho wa Januari,”alisema.

BITEKO ANAVYOUKUBALI

UONGOZI STAMIGOLD

Septemba 19 mwaka huu, Waziri Biteko alitembelea mgodi huo wa Stamigold Biharamulo ambapo alieleza kuridhishwa kwake na unavyoendeshwa na uongozi huo mpya.

“Kwanza wameshusha sana gharama za uendeshaji, mwanzo walikuwa wanazalisha wakia moja kwa dola za Marekani 1,800 na kuiuza kwa dola 1,223, sasa uzalishaji wa wakia moja umeshuka mpaka dola 940.

“Tunaamini wataishusha pia mpaka ifi ke 800 ndipo ambapo tunaweza kupata faida kubwa, lakini wamefanya kazi kubwa kuhakikisha uhai wa mgodi unaweza kuendelea.

“Moja ya hoja inayofanya uendeshaji kuwa juu ni matumizi ya mafuta, tunatumia zaisi ya Sh bilioni moja kwa mwezi kwaajili ya mafuta,

tukipata umeme gharama itashuka, tutakuwa tunatumia Sh milioni

300, tutakuwa tumeokoa karibu Sh milioni 700.

“Wizara ya Madini imeshazungumza na Wizara ya Nishati na kabla ya hapo wakati ikiwa ni wizara moja (Wizara ya Nishati na Madini), mchakato uliokuwepo ni umeme unaotoka Rusumo kwenda Geita tupate line yetu ya megawati tatu ambayo itasambaza umeme kwenye mgodi huu na kushusha gharama za uendeshaji, mradi huu (wa umeme) unakamilika mwakani.

“Kwa wafanyakazi wa mgodi jitihada zao za kupunguza gharama za uendeshaji na kuanza kupata faida, imani yetu ni kwamba wataendelea kuwa waaminifu, tufanye mgodi huu wa Watanzania uwe mfano, tuondoe aibu kwamba Watanzania wakipewa kitu wakisimamie wenyewe kinawafi a mikononi mwao,” anasema Biteko.

Akizungumzia mgodi huo ulivyokuwa kabla kuja kwa uongozi mpya, Biteko anasema “Stangold ilikuwa na historia mbaya sana, mgodi huu ulikuwa shamba la bibi na watu walikuwa wanaiba bila aibu na gharama inabeba Serikali.

Gharama ya mafuta na kemikali ilikuwa inaongezwa mara dufu.

“Serikali iliwekeza Sh bilioni 20 za kuendeleza mgodi lakini matokeo yake mgodi ukazalisha madeni ya Sh bilioni 63 baada ya ukaguzi ikawa Sh

bilioni 45.

“Ilifi ka mahali tukapeleka kwa Rais ombi kutaka mgodi huo uvunjwe, tulisema labda pepo hili linaloitwa Stamigold labuda lifutwe.

Tukaleta timu ya kwanza ikakubali, bahati nzuri Stamico wakajiongeza

wakabadili uongozi.

“Tulivyoleta timu ya pili kukagua tukakuta hali imekuwa angalau nzuri, uzalishaji wa wakii moja umeshuka kutoka dola za Marekani 1,800 hadi 940, tunataka ishuke mpaka 800,”anasema Biteko.

CHIMBUKO LA STAMIGOLD

Mgodi awali ulikuwa ukimilikiwa na Kampuni ya Pangea Minerals, kupitia African Barrick Gold na Januari 2014 Shirika la Madini la Taifa (Stamico) lilikabidhiwa mgodi likiwa na hisa asilimia 99.99 na Msajili wa Hazina

asilimia 0.11.

Stamigold ambayo ni kampuni tanzu ya Stamico, ni ya kitaifa inayokuwa, iliyolenga kuzalisha dhahabu kwa gharama nafuu na kuongeza rasilimali ya muda mrefu wa uwezekano wa biashara huku ikitengeneza fursa za ajira na kuwashirikisha wadau wote kwa maendeleo ya taifa.

Dira yake ni kuwa wazalishaji maarufu wa dhahabu kwa lengo la kuchangia katika uchumi wa taifa na kuwa mfano wa kuigwa sekta ya madini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles