25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Shein: CCM haina mbadala Zanzibar

Dr.-Ali-Mohamed-SheinNa Arodia Peter, Zanzibar

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema chama hicho hakina mbadala wa uongozi, hivyo wananchi wanao wajibu wa kukirudisha madarakani.

Alisema hilo linatokana na uimara wa CCM tangu ilipopata uhuru mwaka 1964 na kuwapo ilani madhubuti zinazowavutia wananchi kila baada ya miaka mitano ya uongozi.

Dk. Shein aliyasema hayo juzi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Bungi, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema ingawa hivi sasa Zanzibar ina  mfumo wa vyama vingi vya siasa, anaamini wananchi bado wanahitaji CCM kuendelea kuongoza dola.

“Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 ndiyo yaliikomboa na kuifanya Zanzibar kuwa huru, bado kuna umuhimu wa CCM kuendelea kutawala na kuenzi mapinduzi hayo.

“CCM inao ujuzi, viongozi makini wenye hekima, uwezo wa kushawishi na kueleweka duniani kuliko chama chochote Tanzania,”alisema Dk. Shein.

Alisema hata kama chama hicho kitashinda uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, kitalazimika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa kuwashirikisha wapinzani ili kulinda matakwa ya Katiba ya Zanzibar.

“Kwa utaratibu tuliojiwekea vyama vitakavyokidhi matakwa ya kikatiba vitalazimika kuunda serikali ya pamoja.

“Mfumo huo, si kwa ajili ya kusababisha vurugu na dhuluma, lengo letu ni kuwa na serikali ya pamoja kwa manufaa ya Wazanzibari,”alisema Dk.Shein.

Alisema CCM inao uzoefu wa kuongoza nchi kwa miaka 51, hivyo wananchi hawapaswi kufanya makosa kuruhusu upinzani kuongoza Zanzibar.

“ Ilani yetu ya mwaka huu ina sura nane zinazoelezea mambo muhimu ya maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar, nina imani nitashinda kwa asilimia nyingi,” alijigamba Dk. Shein.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles