27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Shein awataka vijana kuyalinda mapinduzi

shein.Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

VIJANA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametakiwa kujizatiti zaidi kulinda na kuendeleza mapinduzi ya mwaka 1964 na muungano uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wito huo umetolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na viongozi wa UVCCM Mkoa wa kichama wa Mjini Unguja.

Alisema kuwa kuyalinda na kuyadumisha mapinduzi na muungano ni kulinda na kuendeleza amani na utulivu nchini, hivyo vijana hilo ndilo jukumu lao la msingi kama warithi wa taifa.

“Hakuna mbadala wa mapinduzi, hakuna mbadala wa muungano, wala hakuna mbadala wa amani na utulivu wa nchi yetu, hivyo ni lazima vijana mchukue nafasi yenu kulinda misingi hiyo ya nchi yetu,” alisisistiza Dk. Shein kwa viongozi hao wa vijana kuanzia ngazi ya matawi hadi mkoa.

Alisema ni wakati wao vijana wa sasa kuchukua majukumu hayo kwa kuwa hata wao walikuwa vijana na walihimizwa kufanya hayo hayo na viongozi wao, ndiyo maana wamefanikiwa kukabidhiwa uongozi wa nchi.

“Ni lazima vijana mzingatie historia ya ukombozi wa nchi yenu na ya uongozi wake ndiyo mtaweza kuwa viongozi wazuri na tegemeo la maendeleo ya nchi yenu,” alisema.

Dk. Shein ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alisema vijana ni lazima wasome na kukumbushana mara kwa mara historia ya mapambano ya uhuru wa Zanzibar kwa kuwa ni muhimu katika kujenga mustakabali wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles