27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DK. SHEIN AIPONGEZA WIZARA YA KILIMO

Na Mwandishi Wetu

-PEMBA

UONGOZI wa Mkoa wa Kusini Pemba kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi umepongezwa kwa kuyabainisha na kuyarejesha serikalini mashamba ya Serikali na kuagiza kwa wale wote ambao bado wanayaficha wayarejeshe wenyewe kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.

Hayo yalisemwa jana Kisiwani Pemba na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ambapo alisema aliagiza kuchukuliwa hatua za kisheria bila kujali wadhifa wa mtu, cheo alichonacho au umaarufu wake.

Agizo hilo alilitoa katika majumuisho ya ziara yake aliyoifanya kuanzia Agosti 24, mwaka huu ambapo aliwaagiza viongozi wa mikoa na wilaya kusimamia vizuri ukusanyaji mapato na kushirikiana na wafanyabiashara katika kuwashajiisha ili walipe kodi na kuongeza mapato ya Serikali.

Aliwataka viongozi hao kutojiingiza katika kuwasaidia kukwepa kodi wala kuwakingia kifua kwa makosa yao wanayoyafanya katika kukwepa kulipa kodi.

Pamoja na hali hiyo aliagiza Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kufanya mkutano maalumu na wakuu wa mikoa na wilaya zote za Unguja na Pemba kwa ajili ya kupanga na kupeana majukumu ya utekelezaji wa mpango wa utalii kwa wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles