27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Dk Ngundulile azindua programu kupiga vita mimba za utotoni

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


SERIKALI imeandaa kongamano la taifa lenye lengo la kujadiliana suala la mimba za utotoni na kutoa mapendezo ni kwa namna gani tatizo hilo linaweza kutatuliwa.

Hayo yalisemwa   Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile.

Alikuwa  akizundua programu ya kupinga vita mimba za utotoni ambayo imeandaliwa na Makumbusho ya Taifa kwa udhamini wa Ubalozi wa Uswizi   nchini.

Programu hiyo ina lengo la kuhamamisha jamii  na kutoa elimu madhara yanayotokana na mimba za utotoni kwa watoto wa kike  na kwenye jamii kwa ujumla.

“Tatizo la mimba za utotoni limekuwa likikua kadri siku zinavyokwenda. Ni lazima tufikie mahali tulizungumzie kwenye ngazi ya taifa.

“Hivi karibuni tutazindua kongamano la taifa kuzungumzia tatizo hili ambako tutawahusisha wanasiasa, watunga sheria, viongozi wa dini  na viongozi wa mila,” alisema Dk. Ndungulile.

Alisema mimba za utotoni ni moja ya ukatili wa jinsia na hivyo kama taifa ni lazima tujitokeze na kulizungumzia.

“Wasichana wetu wanakatiza ndoto zao na hasa suala la kujiendeleza katika elimu. Umasikini unazidi kuongeza kwa kuwa wengi wa wasichana wanaopata mimba za utotoni hubaki wakitegemea familia kwa malezi.

“Hili pia inazidi kuongeza umasikini kwenye nchi yetu kwa vile taifa linabaki kuwa watengemezi wengi,” alisema.

Takwimu za taifa za mwaka 2015 zinaonyesha asilimia 27 ya wasichana walio na umri kati ya miaka 15 na 19 wana mimba au wameshazaa kwa mara ya kwanza, hii inaiweka Tanzania kuwa nchi ya tatu barani Afrika kwa ukubwa wa tatizo la mimba za utotoni.

Na takwimu za mkoa zinaonyesha  mikoa ambayo inaongoza kwa tatizo hilo ni Katavi kwa asilimia 45 ikifuatiwa na Tabora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles