22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Ndugulile aeleza kutoridhishwa na utayari wa Kigoma kukabili ebola

Na Mwandishi wetu-Kigoma

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, ametembelea Kigoma kuona utayari wa mkoa huo kukabiliana na ugonjwa wa ebola huku akieleza kutoridhishwa na hali aliyoiona.

Alitembelea bandari kuu ya mkoa, uwanja wa ndege, bandari ndogo ya Kibirizi na Zahanati ya Bangwe ambayo imetengwa maalumu kutoa matibabu kwa mtu atakayebainika kuwa na virusi vya ebola. Dk. Ndugulile alionesha kutoridhishwa na utayari wa mkoa katika kukabiliana na ugonjwa huo, huku akiitaka timu iliyoandaliwa chini ya Mganga Mkuu wa Mkoa, Paul Chaote, kutoa mafunzo kwa timu iliyoandaliwa wajue jinsi ya kujikinga na kutoa huduma kwa mgonjwa atakayebainika.


“Hatuna mgonjwa wa ebola ndani ya nchi, lakini kutokana na hali ya ugonjwa huu katika nchi jirani kuna umuhimu wa sisi kama nchi kuendelea kujipanga na kuhakikisha mifumo yetu yote imekaa vizuri kipindi mgonjwa atakapojitokeza, hivyo nakuomba Mkuu wa Wilaya na Mganga Mkuu wa Mkoa kuendelea kusimamia hili,” alisema Dk. Ndugulile.


Upungufu aliobaini Dk. Ndugulile ni pamoja na wahudumu kutozingatia kanuni walizofunzwa juu ya kujikinga na maambukizi pindi watakapokuwa wakihudumia mgonjwa, kutokuwa na vifaa vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa wa ebola ikiwamo vitanda na watumishi kutokuwa na uelewa na utayari wa kutosha kukabiliana na ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles