DK. MPANGO: TUWASAIDIE WATU WENYE ULEMAVU KUJITEGEMEA

0
790
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango

NA MWANDISHI WETU,

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ameitaka jamii kuwasaidia watu wenye ulemavu ili waweze kujiajiri na kukabiliana na hali ngumu ya maisha.

Dk. Mpango alitoa rai hiyo wakati alipotembelea banda la mlemavu asiyeona, Abdalah Nyangalilo, ambaye amewakusanya watu kadhaa wenye ulemavu na kuwapatia mafunzo ya ushonaji nguo.

Maonyesho hayo ya kwanza ya viwanda vya ndani yanafanyika katika Uwanja wa maonyesho ya biashara wa Mwalimu J. K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Waziri huyo wa Fedha na Mipango, ambaye ametoa msaada wa vyerehani viwili ili kuwaongezea nguvu walemavu hao, alisema watu wenye ulemavu wanaweza kufanya mambo makubwa ya kijasiriamali yatakayowasaidia kujikimu kimaisha, endapo jamii itajitolea kuwasaidia kwa hali na mali.

Kwa upande wake, Nyangalilo, ameiomba Serikali kuanzisha mitaala ya ufundi ukiwamo ushonaji kwenye vyuo vya ufundi hapa nchini ili kuwajengea uwezo watu wenye ulemavu waweze kujitegemea kwa kufanya shughuli za uzalishaji mali badala ya kuwaacha wawe ombaomba.

Maonyesho hayo yanayotarajiwa kufungwa leo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara wa Mwalimu J.K Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam, yamezishirikisha zaidi ya kampuni 400.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here