23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Magufuli, Zungu warusha makombora

MagufuliAziza Masoud na Ruth Mnken, Dar es Salaam
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu (CCM), wamerusha kombora kwa watu wanajipitisha kutaka ubunge Ilala huku wakiwataka watafute kazi za kufanya.
Dk. Magufuli jana alikuwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa barabara za mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), pamoja na kuzindua ujenzi wa barabara ya Kariakoo Msimbazi hadi Karume yenye urefu wa kilometa moja.
Alisema kazi inayofanywa na Zungu imekuwa ikionekana na akawataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua mtu atakayefanya ya kuisimamia Serikali kama Zungu na si wengineo.
“Hawa ambao wanatafuta ubunge kupitia Ilala waambieni waje Tanroads tuwaajiri. Simpigii kampeni lakini inawezekana kabisa ni mtu mwema kwa sababu anaisumbua Serikali kuhakikisha inatekeleza ahadi zake.
“…Zungu oyee… nafikiri sijakosea naweza kuongezea kusema ‘CCM oyee’, kwa sababu hata wapinzani watapita humu,” alisema Dk. Magufuli huku akishangiliwa.
Alisema katika bajeti ya mwaka huu kwa Mkoa wa Dar es Salaam, hatasaini fedha za upanuzi wa barabara kwa mkoa huo endapo Mfuko wa Barabara hautatenga fedha za kutosha kwa ajili ya Manispaa ya Ilala ambayo ina kilomita 1216 tofauti ya maeneo mengine yenye kilomita ndogo.
Waziri lisema barabara hiyo itakayokuwa na njia nne itaanza kujengwa kilomita moja itayoanzia Msimbazi mpaka Karume kwa gharama ya Sh bilioni 2.95.
Akizungumzia Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART) alisema ujenzi huo umeshakamilika kwa asilimia 95 na kuwataka wakandarasi kukabidhi haraka ili Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa(Tamisemi) itafute wawekezaji watakaoleta magari na kuanza kutoa huduma.
Naye Zungu aliwatahadharisha watu wanaotumia mitandao ya jamii ikiwamo Facebook kutafuta ubunge katika jimbo hilo kuachana na mpango huo kwa sababu bado wananchi wanamuhitaji aendelee kuwatumika.
Alisema kuna watu wanahangaika kujitangaza kutaka kugombea jimbo hilo kupitia Facebok bila kujali kuwa anatumia nguvu nyingi kuhakikisha wananchi wa eneo hilo wanapata maendeleo.
“Kuna kiroboto kinapitapita kutaka ubunge kupitia Facebook, majibu ndiyo hayo ‘Fumigation’ ndiyo hii wananchi wanaona mchango wangu katika maendeleo hawawezi kushawishika kwa urahisi,watu bado wana imani na mimi,” alisema Zungu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles